title : AZAM FC YAAHIDI KUTOWAANGUSHA MASHABIKI,WAPO KAMILI KUIVAA SIMBA
kiungo : AZAM FC YAAHIDI KUTOWAANGUSHA MASHABIKI,WAPO KAMILI KUIVAA SIMBA
AZAM FC YAAHIDI KUTOWAANGUSHA MASHABIKI,WAPO KAMILI KUIVAA SIMBA
NAHODHA Msaidizi wa Azam FC, Agrey Moris ameweka wazi kuwa hawatawaangusha mashabiki kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba.
Moris ametoa kauli hiyo ikiwa zimebaki siku mbili kabla ya timu yao ua Azam FC kupambana na Simba.Mchezo huo utakafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ,keshokutwa saa 10 jioni.Ni mchezo unaotarajiwa kuwa mkali ya wa aina yake kutokana na Azam FC iliyojikusanyia pointi 33 kuwa kwenye vita kali ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo dhidi ya wekundu hao walio kileleni kwa pointi 38.
Akizungumzia kuelekea mchezo huo, Moris amewataka mashabiki kuondoa hofu na kuwaomba kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa sapoti.“Kwanza tunamshukuru Mungu wachezaji wako katika morali ya hali ya juu yaani inaonesha wachezaji kila mmoja anajiandaa kuhakikisha kutaka kushinda mchezo huu,” amesema.
Moris amekiri ushindani utakuwa mkubwa kutokana na Simba kuwa kileleni mwa ligi, na kudai kwa sasa timu yake imeongezewa morali kutokana na ushindi wa juzi walipoichapa Ndanda mabao 3-1.“Hiyo inatupa morali zaidi ya kwenda kupambana kwa sababu sisi lengo letu ni kushinda mchezo huu kujihakikishia tunaifukuzia Simba katika nafasi ya juu,” amesema.
Tayari kikosi cha Azam kimeshaanza maandalizi kuelekea mchezo huo na wachezaji wakiendelea kukaa kambini tokea ulipomalizika mtanange dhidi ya Ndanda, yote hiyo ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha inaibuka na pointi zote tatu.Aidha itakumbukwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Azam Complex Septemba mwaka jana, timu hizo zilitoka suluhu.
Ushindi wowote wa Azam FC kwenye mchezo huo, utazidi kupunguza pengo la pointi baina yake na Simba na kufikia mbili na hivyo kuendeleza mapambano ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo, walioutwaa mara ya mwisho msimu wa 2013/2014.
Hivyo makala AZAM FC YAAHIDI KUTOWAANGUSHA MASHABIKI,WAPO KAMILI KUIVAA SIMBA
yaani makala yote AZAM FC YAAHIDI KUTOWAANGUSHA MASHABIKI,WAPO KAMILI KUIVAA SIMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AZAM FC YAAHIDI KUTOWAANGUSHA MASHABIKI,WAPO KAMILI KUIVAA SIMBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/azam-fc-yaahidi-kutowaangusha.html
0 Response to "AZAM FC YAAHIDI KUTOWAANGUSHA MASHABIKI,WAPO KAMILI KUIVAA SIMBA"
Post a Comment