WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA

WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA
kiungo : WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA

soma pia


WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mbinga Mjini, kwenye mkutano wa hadhara aliyouitisha kwenye Uwanja wa Michezo Mbinga Mjini Wilayani Songea, Mkoani Ruvuma. Januari 5, 2018.

*Aagiza uchunguzi ufanyike kuanzia leo, maafisa wa MBICU, MBIFACU kikaangoni
*Apiga marufuku ununuzi wa kahawa kwa mfumo wa MAGOMA
*Aitisha kikao cha wadau wa kahawa Dodoma Jan. 14

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amebaini madudu kwenye Vyama Vikuu vya Ushirika vya Mbinga (MBICU na MBIFACU) na kuagiza uchunguzi ufanyike kuanzia leo.

“Nikiondoka hapa jukwaani, viongozi wote wa zamani na wa sasa waripoti kwa Mkuu wa Wilaya, na OCD hakikisha ofisi za chama hazifunguliwi hadi kesho asubuhi (leo) kazi itakapoanza, ili wasije kubadilisha nyaraka kwenye ofisi yao. Timu yangu ya uchunguzi iko hapa Mbinga, kesho waende wote kwenye ofisi hizo,” alisema huku akishangiliwa na wananchi.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Ijumaa, Januari 5, 2018) wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbinga, kwenye viwanja vya CCM, mjini Mbinga.

“Natambua kuwa MBICU ilishakufa ikiwa na madeni makubwa na mkaunda tena MBIFACU, ambayo nayo inasuasua, lakini viongozi wote hawa watafutwe, waje waonane wa timu  yangu na waeleze fedha za chama zimeenda wapi na kama walizikopea zilifanya nini,” alisisitiza.

Alisema timu hiyo ya uchunguzi itakiangalia chama hicho na kukifumua chote, na wote wakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kinidhamu. “Tunataka MBICU na madeni yenu yaliyoko kwa Msajili wa HAZINA yajulikane, tunataka turudishe hoteli yetu, mashamba yetu na majengo yetu,” alisema.


Hivyo makala WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA

yaani makala yote WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/waziri-mkuu-akemea-madudu-ushirika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA"

Post a Comment