WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE

WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE
kiungo : WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE

soma pia


WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE

*Ataka takwimu za kahawa ziwe tayari ifikapo Feb. 28

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mji na Wilaya za Mbinga wahakikishe kuwa wanaunda kanda za kilimo na kuwasambaza maafisa kilimo wao badala ya kuwaacha wakae maofisini.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Ijumaa, Januari 5, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na Halmashauri ya Mji wa Mbinga, kwenye ukumbi wa Jumba la Maendeleo, mjini Mbinga.

“Mkurugenzi wa TC na DC chuja maafisa kilimo ulionao na uhakikishe wanabakia watatu tu. Abaki DALDO, mtu wa horticulture na mthamini, wengine wote wasambaze kwenye kanda ili wasimamie wakulima wakiwa huko huko. Hili litekelezwe na Mkuu wa Wilaya ulisimamie” alisema.

Aliwataka maafisa kilimo wa zao la kahawa waende vijijini na kufanya sensa ili waweze kubaini wana wakulima wangapi wanaozalisha kahawa. “Afisa kilimo wa wilaya lazima ujue kijiji kina wakulima wangapi wa kahawa, na wana ekari ngapi? Na katika ekari hizo, ana miche mingapi? Hii itaisaidia Serikali ijue inahitaji dawa za aina gani, mbolea kiasi gani na miche mingapi kwa wakulima wake,” alisema.

“Ninataka hizi takwimu ziwe zimekamilika ifikapo tarehe 28 Februari, mwaka huu,” alisisitiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia mche wa Kahawa, wakati alipotembelea kituo cha utafifti wa zao la kahawa (TACRI) kilichopo kwenye kijiji cha Ugano Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dkt. Deusdedit Kilambo. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kitalu cha miche ya Kahawa, wakati alipotembelea kituo cha utafifti wa zao la kahawa (TACRI) kilichopo kwenye kijiji cha Ugano Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dkt. Deusdedit Kilambo na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme Januari 5, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia kahawa kwenye mashine ya kusagia kahawa, wakati alipotembelea kiwanda cha kahawa cha Mbinga Coffee kilichopo Mbinga Mjini Wilayani Songea, Mkoani Ruvuma, kushoto ni Meneja Uzalishaji Rabiel Ulomi na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. Januari 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia sampuli za kahawa kwenye, wakati alipotembelea kiwanda cha kahawa cha Mbinga Coffee kilichopo Mbinga Mjini Wilayani Songea, Mkoani Ruvuma, kulia ni Meneja Uzalishaji Rabiel. Januari 5, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na Watumishi wa Halmashauri ya Mbinga, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma. Januari 5, 2018.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE

yaani makala yote WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/waziri-mkuu-aagiza-maafisa-kilimo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE"

Post a Comment