WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF

WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF
kiungo : WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF

soma pia


WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF

Estom Sanga-Singida 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mhe. George Mkuchika amepongeza hatua ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kubuni utaratibu mzuri wa kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao. 

Mhe. Mkuchika amesema utaratibu huo siyo tu kwamba unapunguza gharama bali unawafanya wananchi kuithamini miradi hiyo na kuitunza kutokana na kutumia nguvu na jasho lao katika kuitekeleza. 

Waziri huyo ameyasema hayo mwishoni mwa juma baada ya kutembelea kijiji cha Mwahango katika halmashauri ya wilaya ya Singida ambako alikagua jengo la zahanati lililojengwa na TASAF kwa kuwashirikisha wananchi kijijini hapo. 

Aidha Mhe. Mkuchika ameupongeza mkoa wa Singida kwa kusimamia zoezi la uandikishaji Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa uaminifu na hivyo kupunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya Watu wasiostahili kujumuishwa kwenye Mpango huo kinyume cha utaratibu. 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika akitoka katika jengo la zahanati ya kijiji cha Mwahango katika halmashauri ya wilaya ya Singida lililojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo. 
Mwonekano wa jengo la zahanati ya kijiji cha Mwahango katika halmashauri ya wilaya ya Singida iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo ikiwa ni mkakati wa TASAF wa kuboresha huduma za Afya kwa walengwa wake na wananchi wa eneo hilo. 
Waziri Mkuchika akipanda mche wa mti katika eneo la Zahanati ya kijiji cha Mwahango katika halmashauri ya wilaya ya Singida iliyojengwa na TASAF na wananchi . 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (aliyesimama mbele ya kamera) akiwahutubia baadhi ya watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Singida wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo. 
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika akikagua jengo la zahanati ya kijiji cha Mwahango katika wilaya ya Singida jengo lililojengwa na TASAF ikiwa ni mkakati wa kuwasogezea huduma ya Afya wananchi na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.





Hivyo makala WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF

yaani makala yote WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/waziri-mkuchika-avutiwa-na-miradi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF"

Post a Comment