VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR

VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR
kiungo : VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR

soma pia


VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR

* Meya wa Temeke, Ubungo nusura kuzichapa
 
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii
VITUKO, Vibweka, vitimbi na kila aina ya kejeli zimetawala wakati wa uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Ilikuwa kama wanaigiza filamu lakini kumbe ndio ilikuwa namna ya kufanya uchaguzi huo ambao kwa sehemu kubwa majibizano yalichukua nafasi kubwa.

Uchaguzi wa kumpata Naibu Meya wa Jiji la Dar es Saalam umefanyika leo mchana na ulihusisha mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mariam Lorida na mgombea wa Chama cha Wananchi(CUF) Mussa Kafana.

ILIKUWA HIVI
Kabla ya uchaguzi huo kufanyika, vibweka, vitimbi na majibizano yalitawala kati ya Vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa)dhidi ya upande wa CCM.

Ukawa hawakuwa tayari uchaguzi huo kufanyika kwani mgombea wao hakuwepo ukumbini huku CCM wakiona ipo haja ya kufanyika uchaguzi wa kumpata Naibu Meya ili shughuli za kimaendeleo zifanyike.

Wakati mjadala huo unaendelea Meya wa Jiji la Dar es Salaam Issaya Mwita hakuwepo ukumbini.Hivyo CCM na Ukawa wakawa wanalumbana aidha kufanyika au kutofanyika uchaguzi huo.
Wakati wanalumbana ziliibuka baadhi ya kauli ambazo CCM hawakuridhika nayo na hasa ile iliyodaiwa kutolewa na Meya wa Ubongo Boniphance Jacob baada ya kudai huenda mgombea wao ametekwa.
Kauli ambayo iliwakera baadhi ya wajumbe wa upande wa CCM na hasa Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo kutaka Jackob afute kauli yake.

MEYA UBUNGO, TEMEKE NUSURA WAZICHAPE
Baada ya matokeo kutangazwa Meya Jackob alimkaba koo Meya wa Temeke Chaurembo.Sababu ni pale Chaurembo alipotaka kusogelea karatasi za kura.

Hivyo kukaibuka malumbano baina ya pande mbili, kiasi cha baadhi  askari polisi waliokuwa wamevaa kiraia kuamua kuingilia kati ili amani iendelee.

UKAWA WASHANGILIA
Matokeo ya uchaguzi huo yaliibua shangwe kwa Ukawa kwani ushindi huo wameamini umemeliza kiu yao ya kuitaka nafasi hiyo.Kwa mujibu wa nafasi ya Naibu Meya kila baada ta miezi sita wanafanya uchagizi.Hivyo Kafana amerudi tena kwenye nafasi hiyo.

CCM WATAFUTA MCHAWI
Ushindi wa mgombea wa Ukawa ukasababisha CCM kuanza kutafuta nani amewasaliti kwani kwa idadi ya washiriki walikuwa idadi sawa.Hivyo kwa matokeo hauo kuna Diwani wa CCM amewasaliti wenzake .Hali iliyoibua maswali.
  Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob  na Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Chaurembo (aliyekaa chini) wakiwa wanaamuliwa na madiwani wengine  wakati wa uchaguzi wa kumtafuta Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam leo ambapo  uchaguzi huo ulijawa visa, vituko na vurugu za hapa na pale.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mussa Kafana (CUF) akiwa amelala ndani ya ukumbi wa Karimjee wakati wa  Uchaguzi wa kumtafuta  Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika leo jijini Dar es salaam na kuibuka mshindi baada ya kumshinda Mariam Rolida diwani wa  CCM kwa kura ya 12 dhidi ya 10.

 Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdalah Chaurembo akizuiwa kuongoza kikao na Diwani wa Chadema Patrick Asenga wakati wa mchakato wa uchaguzi wa kumtafuta Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
 Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (wa kwanza kulia) akizungumza na Madiwani wa Chama cha Mapindzui wakati wa mkutano wa kumtafuta Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam leo.
  Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mussa Kafana akiwa anawasili katika ukumbi wa uchaguzi huku ameshikiliwa na madiwani wenzakeili kuweza  kufanikisha uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR

yaani makala yote VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/vibweka-vituko-vyatawala-uchaguzi-naibu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR"

Post a Comment