title : TPA yanunua vifaa vya kisasa Bandari ya Mtwara
kiungo : TPA yanunua vifaa vya kisasa Bandari ya Mtwara
TPA yanunua vifaa vya kisasa Bandari ya Mtwara
Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imenunua vitendea kazi vipya na vya kisasa kwa ajili ya bandari ya Mtwara ili kuongeza ufanisi.
Vifaa hivyo ambavyo tayari baadhi vimeshawasili bandarini hapo ni pamoja na mzani wa kisasa ‘Movable Weigh Bridge’ wenye uwezo wa kupima hadi tani 100 ambao tayari unatumika.
Vifaa vingine vilivyonunuliwa na vinavyotarajiwa kuwasili kuanzia mwezi Januari, 2018 ni pamoja na ‘Reach Stalker’ mbili mpya zenye uwezo wa kubeba tani 40 kwa wakati mmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko ameyasema hayo wakati wa majumuisho ya ziara za Kamati za Bodi za Wakurugenzi wa TPA zinazoshughulikia TEHAMA na Utelekezaji na ile ya Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara.
Wakurugenzi wa Bodi za Kamati hizo ambazo ziliongozwa na Mwenyekiti, Dkt. Jabiri K. Bakari, ni pamoja na Jayne K. Nyimbo, Renatus Mkinga, Aziz M. Kilonge na Jaffer S. Machano.
Kamati hizo zilitembelea miradi mbalimbali iliyopo Bandari za Mtwara na Lindi na kutoa maelekezo kadhaa ambayo ni muhimu katika kuendeleza bandari hizo ili kuongeza huduma zake.
Akizungumzia vifaa vipya vilivyowasili na vinavyotarajiwa kuwasili hivi karibuni, Mhandisi Kakoko amesema ununuzi wa vifaa hivyo ni utekelezaji wa mipango ya kuifanya bandari hiyo kuwa ya kisasa zaidi.
“Ununuzi wa vifaa tunaofanya sasahivi utasaidia kuboresha na kuimarisha zaidi utendaji kazi wa bandari ya Mtwara na kuongeza ufanisi zaidi,” amesema Mhandisi Kakoko.
Mkuu wa bandari ya Mtwara, Nelson Mlali (Kulia) akitoa maelezo kwa Wakurugenzi wa Bodi wa TPA wa Kamati za TEHAMA na Utekelezaji pamoja na ya Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara mara baada ya wajumbe wa kamati hizo kufanya ziara ya kikazi banddari ya Mtwara hivi karibuni.
Mkuu wa bandari ya Mtwara, Nelson Mlali (Kulia) akitoa maelezo kwa Wakurugenzi wa Bodi wa TPA wa Kamati za TEHAMA na Utekelezaji pamoja na ya Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara mara baada ya wajumbe wa kamati hizo kufanya ziara ya kikazi banddari ya Mtwara hivi karibuni.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TPA yanunua vifaa vya kisasa Bandari ya Mtwara
yaani makala yote TPA yanunua vifaa vya kisasa Bandari ya Mtwara Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TPA yanunua vifaa vya kisasa Bandari ya Mtwara mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/tpa-yanunua-vifaa-vya-kisasa-bandari-ya.html
0 Response to "TPA yanunua vifaa vya kisasa Bandari ya Mtwara"
Post a Comment