title : Mzee Zam apewa Fupa na CAF
kiungo : Mzee Zam apewa Fupa na CAF
Mzee Zam apewa Fupa na CAF
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Mzee Zam Ali kutoka Zanzibar kuwa Kamishna wa mchezo nambari 50 wa kombe la shirikisho kati ya FC Platinum ya Zimbabwe dhidi ya Club Desportivo 1 de Agosto ya Angola mchezo utakaopigwa 20 au 21 ya February, 2018 huko Zimbabwe.
Mzee Zam atawasimamia Waamuzi wa Afrika ya Kusini watakaochezesha mchezo huo akiwemo muamuzi wa kati Christopher Harrison, akisaidiwa na muamuzi namba moja Sandile Dilikane na muamuzi namba mbili Thembisile Theophilus huku Muamuzi wa akiba akiwa Tinyiko Victor Hlungwani.
“Nimefurahi CAF kuendelea kuwa na imani na mimi kwani wananijua vyema hasa hivi karibuni nilikuwa Kamishna katika Mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup yaliofanyika nchini Kenya, mimi ni mzoefu kuchaguliwa kwenye shughuli za soka kama hizi katika Mashindano mbali mbali”. Alisema Mzee Zam.
Hivyo makala Mzee Zam apewa Fupa na CAF
yaani makala yote Mzee Zam apewa Fupa na CAF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mzee Zam apewa Fupa na CAF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/mzee-zam-apewa-fupa-na-caf.html
0 Response to "Mzee Zam apewa Fupa na CAF"
Post a Comment