title : MHALIFU ATAINGIA DAR AKIWA SALAMA LAKINI HATATOKA SALAMA-MAMBOSASA
kiungo : MHALIFU ATAINGIA DAR AKIWA SALAMA LAKINI HATATOKA SALAMA-MAMBOSASA
MHALIFU ATAINGIA DAR AKIWA SALAMA LAKINI HATATOKA SALAMA-MAMBOSASA
*Asema wamedhibiti uhalifu, azungumzia Panya road
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KAMANDA wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema iwapo kuna mhalifu yoyote na wa kutoka sehemu yoyote anaweza kuingia Dar es Salaam salama lakini ajue hatatoka salama.
Amefafanua kutoka na kujipanga vema kulinda usalama wa raia na mali zao kwa Jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa kukomesha uhalifu na hata waliokuwa wanajiita Panya Road na makundi mengine ya kihalifu sasa imebaki historia huku akifafanua jeshi hilo halipo tayari kuchezewa.
Mambosasa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea tuzo maalumu iliyotolewa na uongozi wa Redio Times Fm na kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kama sehemu ya kutambua mchango wanaoutoa katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wakati wote.Tuzo hiyo ilitolewa na Mkurugenzi .
Mtendaji wa redio hiyo Rehule Nyaula.Amesema tuzo hiyo imewatia moyo polisi Kanda Maalumu kwani imekuwa ni kawaida kusikia tu wakilaumiwa lakini Redio Times wanatambua kazi ambayo wanafanya na kuomba wengine kuiga mfano huo wa kuthamini kazi zinazofanywa na taasisi mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Times FM, Rehule Nyaulawa(aliyesimama)akizungumza leo akiwa katika Ofisi za Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kabla ya kukabidhi tuzo maalum ambayo inalenga kutambua mchango wa Polisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akionesha tuzo maalum ambayo wamepewa na Radio Times FM.Tuzo hiyo ni kutambua mchango wa Polisi katika kulinda usalama wa wananchi wa Dar es Salaam kwa mwaka 2017
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa(aliyesimama) akizungumza leo kabla ya kupokea tuzo maalum ya kutambua mchango wao katika suala la ulinzi na usalama iliyotolewa na uongozi wa Radio Times FM wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Rehule Nyaula(aliyekaa kushoto) .
Hivyo makala MHALIFU ATAINGIA DAR AKIWA SALAMA LAKINI HATATOKA SALAMA-MAMBOSASA
yaani makala yote MHALIFU ATAINGIA DAR AKIWA SALAMA LAKINI HATATOKA SALAMA-MAMBOSASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MHALIFU ATAINGIA DAR AKIWA SALAMA LAKINI HATATOKA SALAMA-MAMBOSASA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/mhalifu-ataingia-dar-akiwa-salama.html
0 Response to "MHALIFU ATAINGIA DAR AKIWA SALAMA LAKINI HATATOKA SALAMA-MAMBOSASA"
Post a Comment