title : Masogange anendelea kukwamisha kesi yake
kiungo : Masogange anendelea kukwamisha kesi yake
Masogange anendelea kukwamisha kesi yake
ANDE wa mashitaka katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes Gerald maarufu kama ‘Masogange’ umeiomba Mahakama kuuonya upande wa utetezi kwa kushindwa kutoa ushahidi wao kwa mara ya tatu mfululizo
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri kuwa Wakili mwenzake anayemtetea Mshtakiwa Msogange, Reuben Simwanza, ndiye aliyeandaa mashahidi lakini ameshindwa kufika kwa kuwa anaumwa.
Nkoko amongeza, atahakikisha anaandaa mashahidi ili ikitokea wakili mmoja wao hayupo, mwengine aendelee na kesi.Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alidai kuwa hawana pingamizi na sababu zilizotolewa na upande wa utetezi lakini wanaomba mahakama itambue kuwa ni mara ya tatu kesi kwa upande wa utetezi inaahirishwa.
"Mawakili wapo wengi lakini wanashindwa kuendelea kutoa ushahidi wao wa upande wa utetezi basi kama hawawezi, waache mshitakiwa aendelee na kesi mwenyewe," alidai Kakula.Pia aliiomba mahakama kutoa ahirisho la mwisho kwa sababu kesi ni ya muda mrefu. Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.
Masogange ataanza kujitetea baada ya mahakama kumkuta na kesi ya kujibu baada ya kusikiliza mashahidi watatu wa upande wa mashitaka.
Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, mwaka jana katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
Pia anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
Hivyo makala Masogange anendelea kukwamisha kesi yake
yaani makala yote Masogange anendelea kukwamisha kesi yake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Masogange anendelea kukwamisha kesi yake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/masogange-anendelea-kukwamisha-kesi-yake.html
0 Response to "Masogange anendelea kukwamisha kesi yake"
Post a Comment