FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!?

FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!? - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!?, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!?
kiungo : FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!?

soma pia


FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!?

 Na Hafidh Kido, Moshi.

KWA nafasi yangu ya msemaji wa timu ya Coastal Union 'Wagosi wa Kaya' ninatakiwa kusafiri na timu popote iendapo lakini kutokana na majukumu mengine nashindwa kutenda haya.

Lakini nilijiapiza mechi baina ya Wagosi na Polisi Tanzania iliyochezwa mjini Moshi katika uwanja wa Chuo cha Ushirika lazima niende. Kwa bahati ikatokea dharura ya kifamilia nikapata ruhusa kibaruani nami nikahudhuria.

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwepo na maneno kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), anaikingia kifua Coastal Union kwa sababu ni mwenyeji wa Tanga lakini pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za kiuongozi kwenye klabu hiyo kongwe ya jijini Tanga iliyoanzishwa mwaka 1948.

Kama hiyo haitoshi ikaelezwa kuwa kikosi cha Coastal Union kinacheza soka kwa kubebwa waamuzi ambao wanapokea maagizo kutoka TFF.

Yamezungumzwa mengi, itoshe tu kusema baadhi ya klabu zinazoshiriki Ligi ya soka Daraja la kwanza wamekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kudai Coastal Union inabebwa.

Nimeamua kuja kushuhudia 'kubebwa' kwa Coastal Union. Naomba nitangaze maslahi kabla sijaendelea na andiko hili nililoliandika saa nane usiku wa kuamkia Jumapili Januari 21, 2018 nikiwa chumba cha hoteli Mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

Mimi ni shabiki wa Coastal Union lakini pia ni mwanahabari. Hivyo naandika kwa jicho la kihabari lakini naweza kuteleza nikaweka unazi katika andiko hili. Nipo tayari kukosolewa na hata kuzodolewa ikiwa nitaandika uongo au kuongeza chumvi.

Hadi naandika haya msimamo wa kundi B inayojumuisha timu nane yaani Coastal Union, Polisi Tanzania, JKT Mlale, Kinondoni Manicipal (KMC), Mbeya Kwanza, Mufindi United, Mawenzi Market na Polisi Dar es Salaam.

Coastal Union ilikuwa inaongoza kundi kwa jumla ya alama 22, ikifuatiwa na Polisi Tanzania (21), JKT Mlale (21), KMC (19), Mbeya Kwanza (16), Mufindi Utd (12), Mawenzi Market (7) na Polisi DSM (3).

Kwa namna yoyote ile Polisi Tanzania wameumizwa na suluhu tuliyowalazimisha katika uwanja wao. Hivyo walijiandaa kwa hali yoyote iwayo kuhakikisha tunawaachia alama tatu muhimu kwao ili kujihakikishia kupanda Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.



Hivyo makala FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!?

yaani makala yote FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!? mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/figisu-figisu-kama-hizi-kwenye-soka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "FIGISU FIGISU KAMA HIZI KWENYE SOKA LETU,MPAKA LINI.!?"

Post a Comment