title : CUBA YAKUBALI KUSOMESHA MADAKTARI KUTOKA ZANZIBAR
kiungo : CUBA YAKUBALI KUSOMESHA MADAKTARI KUTOKA ZANZIBAR
CUBA YAKUBALI KUSOMESHA MADAKTARI KUTOKA ZANZIBAR
Serikali ya Jamuhuri ya Cuba imetiliana Saini Mkataba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Usomeshwaji wa Madaktari Wazalendo 15 wa Zanzibar Nchini Cuba katika Fani ya Shahada ya Uzamili ya Udaktari.
Madaktari hao 15 ambao Wanane wa Mwanzo wataanza Mafunzo yao Mwezi ujao wakifuatiwa na wengine 7 wa awamu ya Pili ni Miongoni mwa Wanafunzi waliomaliza masomo yao kupitia mpango wa masomo ulioasisiwa kati ya Serikali ya Cuba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Saini ya Mkataba huo kwa Serikali ya Cuba imewekwa na Balozi wa Nchi hiyo Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernades na kwa upande wa Zanzibar Saini ikatiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Halima Maulid Salum.
Hafla hiyo fupi ya Kihistoria imeshuhudiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyejumuika pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Wizara husika, Watendaji wa Wizara hizo na kufanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Kushoto na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bibi Halima Maulid Salum wakisaini Mkataba wa Usomeshwaji wa Madaktari Wazalendo 15 wa Zanzibar Nchini Cuba katika Fani ya Shahada ya Uzamili ya Udaktari.Nyuma yao ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na aliye simama mbele yao ni msaidizi wa Balozi wa Cuba Meylin Suarez.
Profesa Lucas Domingo Kushoto na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bibi Halima Maulid Salum wakibadilishana nyaraka za Mikataba mara baada ya kusaini.
Balozi Lucas Domingo akizungumza kabla ya utiaji saini kwenye Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyopo Vuga Mjini Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Afya Zanzibar Mheshimwa Mahmoud Thabit Kombo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar na ule wa Ubalozi wa Cuba Nchini Tanzania. Kulia ya Balozi Seif ni Balozi wa Cuba Prifesa Lucas Domingo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moha’d Aboud Moha’d, Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo na Msidizi wa Balozi Cuba Nchini Tanzania Bibi Meylin Suarez.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala CUBA YAKUBALI KUSOMESHA MADAKTARI KUTOKA ZANZIBAR
yaani makala yote CUBA YAKUBALI KUSOMESHA MADAKTARI KUTOKA ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CUBA YAKUBALI KUSOMESHA MADAKTARI KUTOKA ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/cuba-yakubali-kusomesha-madaktari.html
0 Response to "CUBA YAKUBALI KUSOMESHA MADAKTARI KUTOKA ZANZIBAR"
Post a Comment