title : BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI.
kiungo : BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI.
BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI.
Na Joel Maduka-Geita.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko amewataka wachimbaji ambao wanamiliki leseni kuhakikisha wanazingatia sheria ambazo wamepewa likiwemo suala la kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwenye maeneo yao ya mgodi ili kuepukana na majanga ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwenye shughuli za uchimbaji.
Akizungumza wakati alipotembelea na kutoa pole kwenye mgodi mdogokijiji cha Buntubili eneo ambalo hivi karibuni mchimbaji mmoja aliangukiwa na kifusi na kufariki.Naibu waziri Doto alisema ni vyema kwa kila mwenye leseni kuhakikisha usalama unakuwa ni jambo la kwanza huku akimwagiza afisa madini kufuatilia migodi yote kama imewekwa mabango ambayo yanaelekezea suala la usalama kwenye mazingira hayo.
“Hatutaki kuona hata mtanzania mmoja anakufa katika mazingira ya uzembe tunatamani tuone watanzania wote wanachimba wanaendeleza mali na wanabaki kuwa salama kwaajili ya kulihudumia Taifa hili ,Taifa hili linawaitaji watu wote kwa hiyo nitoe wito kila mwenye leseni maali popote alipo ahakikisha kwamba mazingira yake ya kazi usalama kiwe kipaumbele na sasa kuanzia leo afisa madini ninakuagiza wote wenye leseni ambao wanaendeleza migodi waweke mabango yanayoeleza umuhimu wa usalama kila kwenye mgodi unaofanya kazi”Alisisitiza Mh,Doto.
Pamoja na hayo Naibu Waziri wa Madini amewataka wananchi kutokuingia kwenye maeneo ambayo yamesimamishwa na ambayo ni hatarishi kwani kufanya hivyo wanaweza kujisabasha hatari ya kupoteza maisha kutokana na maeneo hayo kutokuwa kwenye hali nzuri ya uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko,Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Buntumbili Wilayani Bukombe ambapo kulitokea tukio la mchimbaji kufukiwa na kifusi wakati alipokuwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko pamoja na viongozi wa Wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye eneo ambalo ajali ya mchimbaji kufukiwa na kifusi ilitokea
Baadhi ya viongozi na Naibu waziri wa madini Doto Biteko wakiwa kwenye shimo ambalo ndipo mchimbaji mdogo ambaye alipoteza uhai wakati akiwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko akipatiwa maelezo ya namna ajali hiyo ilivyotokea mgodini hapo.
Mmiliki wa mgodi huo,akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa madini namna ambavyo wachimbaji hao walivyovyamia eneo hilo na kuanza shughuli za uchimbaji hali ambayo imesababisha mmoja wao kufukiwa na kifusi.
Hivyo makala BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI.
yaani makala yote BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/biteko-awataka-wachimbaji-wadogo.html
0 Response to "BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI."
Post a Comment