Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais

Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais
kiungo : Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais

soma pia


Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais


Na Florah Raphael.

Wafanyabiashara wadogowadogo wanaofanya biashara kwenye stendi ya mabasi yaendayo mikoani wamefanya maandamano madogo wakishinikiza na kupinga manyanyaso dhidi ya wafanyabiashara huku lawama kubwa zikienda kwa meneja wa stendi hiyo Imani E. Kasagala.

Akiongea na wandishi wa habari katika mkusanyiko huo, katibu wa umoja wa wafanyabiashara Ubungo John Shayo amesema kuwa walipewa idhini ya kufanya biashara ndani ya stendi hiyo na meya ikiwa ni kuunga mkono kauli ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya hapa kazi tu pamoja na amri yake ya kuwaacha wafanyabiashara wadogowadogo kufanya biashara kwa uhuru pasipo kubuguziwa.

Pia Shayo ameongeza kuwa pamoja na tamko la Rais imekuwa tofauti kwa meneja huyo kwani amekuwa na manyanyaso yasiyo na sababu za msingi na amekuwa na kauli mbaya pindi wanapomuhitaji kwaajili ya mazungumzo hivyo wanamuomba meya wa jiji kushughulikia tatizo hili ili waijue hatima yao ni ipi.

“Hili tatizo ni la mda mrefu hivyo tunamuomba meya wa jiji aje atoe tamko rasmi ili tujue hatima yetu ni IPI” amesema Shayo.Pia Shayo amesisitiza kuwa lengo lao ni kufanya kazi hivyo hawatayafumbia manyanyaso ya meneja huyo hadi meya atakapokuja kufanya maamuzi tena wakiwa pamoja na meneja huyo ili Haki itendeke.“Lengo letu ni kufanya kazi “hapa kazi tu” hivyo hatutakufumbia macho jambo hili hadi meya atakapokuja kufanya maamuzi tena wakiwa pamoja na meneja huyo ili Haki itendeke” amesema Shayo.

Aidha pia mfanyabiashara mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Japhari Hatibu ambaye ni mwenyekiti wa watembeza mikate ndani ya stendi amesema kuwa wafanyabiashara wanapigwa faini bila kosa na hakuna lisiti inayotolewa na anayeshindwa kutoa faini hupelekwa rumande.Pia Hatibu ameongeza kuwa pamoja na kutozwa faini pia Wapo wamama wajane wanaotegemea biashara hiyo ili kulisha familia zao hivyo wanakuwa katika wakati mugumu na itapelekea watu kujihusisha na biashara zisizofaa endapo hali hiyo itaendelea.

Kwa upande wake meneja kasagala aliyetupiwa lawama hizo amejibu tuhuma hizo kwa kusema kuwa kituo kinaendeshwa na sheria ndogo ambayo marekibisho wamefanya mwaka 2009 ambapo sheria hiyo ilikuwa inatumika toka mwaka 2004.

Akifafanua sheria hiyo meneja huyo amesema kuwa biashara zozote zinazotembezwa haziruhusiwi ndani ya kituo na kuongeza kuwa wanaoruhusiwa kuonekana ndani ya kituo ni wanaohusika na mambo ya usafiri pamoja na wafanya biashara wanaotambulika na wale walioko kwenye mfumo maalumu, kama vile wenye maduka na wenye vibali maalum.

“Wanaoruhusiwa kuonekana kwenye kituo ni wanaohusika na mambo ya usafiri pamoja na wafanya biashara wenye vibali maalum na walioko kwenye mfumo maalumu kama wale wenye maduka” amesema Kasagala.


Baadhi ya wafanyabiashara wadogowadogo wanaofanya biashara zao katika eneo la stendi ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo, wakiwa wameshikilia mabango yenye kupinga manyanyaso yanayoendelea dhidi yao.


Hivyo makala Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais

yaani makala yote Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/wafanyabiashara-wadogowadogo-ubungo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais"

Post a Comment