title : VIONGOZI WA UMMA WAPIGANAVIKUMBO KUREJESHA FOMU SECRETARIETI YA MAADILI.
kiungo : VIONGOZI WA UMMA WAPIGANAVIKUMBO KUREJESHA FOMU SECRETARIETI YA MAADILI.
VIONGOZI WA UMMA WAPIGANAVIKUMBO KUREJESHA FOMU SECRETARIETI YA MAADILI.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala mhe. Sophia Mjema akiwa nje ya ofisi za Secretarieti ya Maadili mara baada ya kuwasilisha fomu zake katika Secretariet ya Maadili ya viongozi wa umma.
Mwambawahabari
Na John Luhende
Secretariet ya maadili ya viongozi wa umma imesema imewataka viongozi wa umma ambao hawajarejesha from zao za tamko la Rasilimalia Mali na madeni, kufanya haraka kwakuwa mwisho wa muda uliowekwa ni tarehe 31 Dec 2017.
Akizungumza na wanahabari Kamishna wa Maadili secretariet ya maadili ya viongozi wa umma Jaji mstaafu Harold Nsekala , amesema ofisi za secretariet hiyo zitakuwa Wazi hadi siku ya Jumamosi tarehe 30 kuanzia saa 2.00asubuhi hadi jion saa 10ili kufanikisha zoezi hilo.
Amezitaja ofisi za kanda kuwa ni, kanda ya kati Dodoma, kanda ya ziwa Mwanza, kanda ya Nyanduga za juu kusini Mbeya, kanda ya Kusini Mtwara, kanda ya Magharibi Tabora, kanda ya kaskazini Arusha na Kanda ya Mashariki Kibaha.
Mwambawahabari, imepigakambi katika ofisi hizo na kushuhudia viongozi wakipiganavikumbo kurejesha fomu hizo, mkuu wa Wilaya ya Ilala mhe. Sophia Mjema mara baada ya kurejesha fomu zake amemshukuru Rais kwa kuongoza viongozi na kuonyesha mfano na amemshukuru ofisini hiyo kwa mapokezi mazuri pamoja na ubora wa huduma zao, na akawataka viongozi kuzingatia muda wa kurudisha fomu na kujipanga kwa mara nyingine wa zingatia kwa kurejesha fomu mapema zaidi kuliko kusubiria tarehe za mwisho.
Baadhi ya viongozi wengine waliofika kurejesha fomu hizo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi , Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Mbunge Gulamali wa Manonga Tabora, Mbunge wa Ubungo Said Kubenea, hata hiyo viongozi wengi walituma wawakilishi wao.
Hivyo makala VIONGOZI WA UMMA WAPIGANAVIKUMBO KUREJESHA FOMU SECRETARIETI YA MAADILI.
yaani makala yote VIONGOZI WA UMMA WAPIGANAVIKUMBO KUREJESHA FOMU SECRETARIETI YA MAADILI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI WA UMMA WAPIGANAVIKUMBO KUREJESHA FOMU SECRETARIETI YA MAADILI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/viongozi-wa-umma-wapiganavikumbo.html
0 Response to "VIONGOZI WA UMMA WAPIGANAVIKUMBO KUREJESHA FOMU SECRETARIETI YA MAADILI."
Post a Comment