TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI

TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI
kiungo : TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI

soma pia


TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI

NA VICTOR MASANGU, MKURANGA 

MAMLAKA ya mapato (TRA) Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani imefanikiwa kukamata tani 26 za mizigo ya aina mbali mbali ambayo ilikuwa imepakizwa katika malori mawili ya magari ikisafirishwa kinyemela kutokea kariakoo Jijini Dar es Salaam kuelekea mikoa ya kusini bila ya kuwa na risiti halali kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa TRA Wilaya ya Mkuranga Amosie Ernest alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa baada ya kuyakamata malori hayo walipoyapekuwa waliweza kubaini kuwa yamesheheni bidhaa nyingi ambazo hazijakatiwa risiti kwa mfumo wa mashine ya kielectroniki (EFD), hivyo walikuwa wanakwepa kulipa kodi.

“Ni kweli kwa sasa tupo katika msako mkali kwa ajili ya kuweza kugagua magari yote ambayo yanabeba miigo bila ya kuwa na risiti, na katika zoezi hili tumefanikiwa kuyakamata magari mawili makubwa ambayo yalikuwa yamebebeba mzigo ambao ulikuwa na bidhaa mbali mbali na baada ya kufanya uchunguzi tuliweza kuona kuwa kuna mapungufu makubwa kutokana na wahusika kutokuwa na risiti hivyo magari tumeyakamata yote,”alisema Ernest.

Pia alisema kwamba mizigo hiyo ambayo ilikuwa inasafirishwa kutokea maeneo ya kariakoo Jijijini Dar es Salaam kuelekea mikoa ya kusini ilikuwa na mapungufu makubwa kutokana na baadhi ya mizigo mingine ilikuwa haina risiti kabisa na baadhi ya mingine ilikuwa imekatiwa risiti kwa gharama ambayo ni ndogo ukilinganisha na bei iliyonunuliwa dukani.

Kwa upande wake Afisa elimu na huduma kwa mlipa kodi wa TRA Mkoa wa Pwani Kapera Bakari amebainisha kuwa thamani ya awali ambayo wameifanya wamebaini mizigo hiyo ambayo ina jumla ya thamani ya shilingi milioni 84 imekwepa kulipiwa kodi kihalali ni zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 16 ambazo zilitakiwa kuingia serikalini.

Aidha Kapera alibainisha kuwa serikali ya awamu ya tano kwa sasa ipo macho katika kuhakikisha inakusanya mapato yake hivyo amewaasa wafanyabiashara wote Mkoa wa pwani kuachana na tabia ya kununua mizigo dukani bila ya kuwa na risiti ya aina yoyote kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kupoteza mapato kutokana na tabia ya ukwepaji wa kulipa kodi kwa kutumia mashine za EFD.

Mmoja wa madereva ambaye amekamatwa kutokana na kuhusika na tukio hilo ajulikanaye kwa jina la Hamis Abibu amesema kwamba mizigo ambayo alikuwa ameipakia katika gari yake akutambua lolote kama imenunuliwa bila ya kuwa na risiti ambazo zinastahili.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Sevelini Lalika ambaye nae alifika katika eneo la tukio ameipongeza TRA kwa juhudi wanazozifanya za kumuunga Rais wa awamu ya tano Dk,John Pombe Mgaufuli katika kuhakikisha wanakusanya kodi ipasavyo na kuwabana wale wote wenye tabia ya kukwepa kulipa kodi ya serikali kwa makusudi.

MALORI hayo mawili ya magari ambayo yamekamatwa na TRA yamekutwa yamesheheni bidha mbali mbali zikiwemo mikeka, viatu, mashuka, baiskeli,sabuni, spea mbali mbali za pikipiki, zimeingiza hasara ya zaidi ya kisi cha shiingi milini 16 kutokana na kukwepa kulipa kodi kihalali.


Hivyo makala TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI

yaani makala yote TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/tra-mkoani-pwani-yanasa-tani-26-za.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TRA MKOANI PWANI YANASA TANI 26 ZA MIZIGO AMBAYO ILIKUWA IKISAFIRISHWA KINYEMELA BILA YA KUWA NA RISITI"

Post a Comment