title : TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER YAZIDI KUJIFUA KUJIANDAA NA MICHUANO YA COPA DAR ES SALAAM
kiungo : TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER YAZIDI KUJIFUA KUJIANDAA NA MICHUANO YA COPA DAR ES SALAAM
TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER YAZIDI KUJIFUA KUJIANDAA NA MICHUANO YA COPA DAR ES SALAAM
Kocha wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni, John Mwansasu ameita kikosi cha wachezaji 16 walioingia kambini mwishoni mwa wiki iliyopita kujiandaa na michuano ya Copa Dar es Salaam itakayofanyika kwa siku mbili kwenye fukwe ya Coco.
Kikosi hicho cha wachezaji 16 kimeingia kambini kwa muda wa wiki moja ikiwa ni kujiandaa na mashindano hayo ya kimataifa yatakayojumuisha timu nne ambazo ni Malawi, Uganda, Zanzibar na wenyeji Tanzania Bara.
Wachezaji walioitwa ni pamoja na Rajabu Ghana (Huru), Khalifa Mgaya (Chuo cha CBE), Juma Kaseja (Kagera Sugar), Juma Sultan (Chuo Kikuu Ardhi), Ally Rabby (Huru), Mwalimu Akida (Huru), Samwel Salonge (Huru), Athuman Idd 'Chuji' (Coastal Union) na Kenan Mwandisi (Huru).
Wengine ni John Pauseke (Huru), Joseph Jafet (Huru), Jaruph Rajab Juma (Chuo cha DIT), Mbwana Mshindo (Chuo cha DSJ), Rolland Msonjo (Singida United), Jerry Francis Robert (Huru) na Haruna Moshi (Friends Rangers)
Benchi la ufundi linaongozwa na Mwansasu mwenyewe akisaidiwa na kocha wa makipa Peter Manyika, Meneja Deo Lucas na daktari wa timu Richard Yomba.
Kocha John Mwansasu amesema mashindano hayo ya Copa Dar es Salaam yatakayofanyika Desemba 25 na 26, 2017 yatasaidia kuwaongezea uzoefu zaidi katika mchezo huo wa soka la ufukweni.
Timu ya Taifa ya Beach Soccer ikiendelea na mazoezi kwenye Ufukwe wa Coco kujiandaa na mashindano ya kimataifa ya Copa Dar Es Salaam yatakayofanyika Desemba 25-26 mwaka huu kwenye Ufukwe wa Coco.
Hivyo makala TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER YAZIDI KUJIFUA KUJIANDAA NA MICHUANO YA COPA DAR ES SALAAM
yaani makala yote TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER YAZIDI KUJIFUA KUJIANDAA NA MICHUANO YA COPA DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER YAZIDI KUJIFUA KUJIANDAA NA MICHUANO YA COPA DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/timu-ya-taifa-ya-beach-soccer-yazidi.html
0 Response to "TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER YAZIDI KUJIFUA KUJIANDAA NA MICHUANO YA COPA DAR ES SALAAM"
Post a Comment