title : TANESCO Yawatoa Hofu Wateja Wake Juu Ya Mfumo Wa Ununuzi Wa Luku
kiungo : TANESCO Yawatoa Hofu Wateja Wake Juu Ya Mfumo Wa Ununuzi Wa Luku
TANESCO Yawatoa Hofu Wateja Wake Juu Ya Mfumo Wa Ununuzi Wa Luku
Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa Umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua
katika mifumo iliyozoeleka.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA) wa Tanesco, Demetruce Dashina alisema kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakihamisha mitambo hiyo kutoka ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.
“Jana tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwenda katika ofisi zetu mpya hivyo ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba(jana) mfumo huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundi” alisema Dashina
Alisema kuwa shirika lilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa kuhamisha mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo kufanya mfumo wa
ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko Kawaida.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji aliwaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.
Muhaji alisema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo kuwataka watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya kuwahudumia kama inavyohitajika.
Hivyo makala TANESCO Yawatoa Hofu Wateja Wake Juu Ya Mfumo Wa Ununuzi Wa Luku
yaani makala yote TANESCO Yawatoa Hofu Wateja Wake Juu Ya Mfumo Wa Ununuzi Wa Luku Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANESCO Yawatoa Hofu Wateja Wake Juu Ya Mfumo Wa Ununuzi Wa Luku mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/tanesco-yawatoa-hofu-wateja-wake-juu-ya_11.html
0 Response to "TANESCO Yawatoa Hofu Wateja Wake Juu Ya Mfumo Wa Ununuzi Wa Luku"
Post a Comment