title : RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI AWASILI MKOANI DODOMA NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI
kiungo : RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI AWASILI MKOANI DODOMA NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI
RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI AWASILI MKOANI DODOMA NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Hassan Suluhu,Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt.Augustine Mahiga ,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Dkt Bilinith Mahenge wakiwa uwanja wa Ndege wa Dodoma kumpokea Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi.
Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi akishuka kutoka katika ndege iliyomleta katika uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akimtambulisha Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi kwa viongozi mbalimbali wa Serikali waliofika katika uwanja wa Ndege wa Dodoma kumpokea.
Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliofika kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakipita kwenye gadi ya Heshima iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi mara baada ya Rais huyo wa Msumbiji kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za utamaduni mara baada ya Rais huyo wa Msumbiji kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakati vikundi vya ngoma vilipokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi katika Ikulu ya Dodoma kabla ya kuanza mazungumzo yao.
PICHA NA IKULU
Hivyo makala RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI AWASILI MKOANI DODOMA NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI
yaani makala yote RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI AWASILI MKOANI DODOMA NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI AWASILI MKOANI DODOMA NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/rais-wa-msumbiji-filipe-nyusi-awasili_14.html
0 Response to "RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI AWASILI MKOANI DODOMA NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI"
Post a Comment