Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA

Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA
kiungo : Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA

soma pia


Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ashasta Nditye, ametoa siku 14 kuhakikisha bomba la mafuta la Kimataifa linalosambaza mafuta (TIPPER), liwe limeunganishwa kwenye mfumo unaodhibitiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili serikali iweze kupata mapato sahihi.

Kutokana na bomba la tipper kuunganishwa katika bandari kumesababisha serikali kupata mapato kwa kampuni hiyo kujisimamia yenyewe.

Akizungumza katika ziara ya kikazi aliyoifanya bandarini hapo jana,  Nditye amesema, TPA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na EWURA wafanye uchunguzi wa haraka kufahamu upotevu wa mapato ya serikali yaliyotokana na Tipper kujiunganishia mafuta kutoka kwenye meli bila kupitia katika kituo cha Kurasini Oil Jet (KOJ).

Amesema Tipper  wamekiuka maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaaliwa yaliyolewa Februari mwaka jana  ya kutaka waunganishe bomba lao katika mfumo wa TPA ili kufahamu kiwango cha mafuta wanayoyachukua.

" Wizi wa waziwazi  tangu Februari mwaka jana alipoagiza Waziri  Mkuu  hadi leo TIPPER mmeshindwa kuunganisha bomba lenu hali inayochangia mapato ya Serikali kuzidi kupotea," alisema Nditye.

Amesema TIPPER waliagizwa na waziri ndani ya mwezi.mmoja wawe wamejiunga katika.mfumo huo lakini cha ajabu maaagizo yamekiukwa hali inayoashiria bado kuna ujanja unaendelea.

Amesema haiwezekani TIPPER wakajiunganisha wenyewe halafu wakajisimamia wao.kufahamu kiwango cha mafuta ya dizeli na ya kula wanayotumia.

Aliagiza pia TPA iimarishe ulinzi kwa mtoa taarifa za upotevu wa mafuta hayo na endapo atapata madhara Serikali.itachukua hatua.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditye akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) katika ziara yake alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini  (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko  akitoa taarifa za utendaji wa mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditiye (Kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mamlaka ya Bandari jijini Dar es Salaam.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditiye akizungumza katika ujenzi wa scanner ya ukaguzi katika bandari ya Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA

yaani makala yote Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/naibu-waziri-nditiye-atoa-siku-14-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA"

Post a Comment