title : Naibu Waziri Mgalu Awataka Wakandarasi Tanga kutoa Maelezo Ya kutokuanza Miradi
kiungo : Naibu Waziri Mgalu Awataka Wakandarasi Tanga kutoa Maelezo Ya kutokuanza Miradi
Naibu Waziri Mgalu Awataka Wakandarasi Tanga kutoa Maelezo Ya kutokuanza Miradi
Na Greyson Mwase, Tanga
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amezitaka kampuni za Derm Electric, Njarita, Agwilla na Radi Services kutoa maelezo kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ya kutokuendelea na kazi katika maeneo yao ya miradi wakati walikwishalipwa malipo ya awali na Serikali.
Mgalu alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki tarehe 16 Desemba, 2017 alipofanya kikao na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)- Ofisi ya Tanga baada ya kubaini wakandarasi hao hawapo katika maeneo hayo ya kazi na kutohudhuria kikao hicho kama alivyoagiza.
Kikao hicho kilishirikisha pia watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Alisema kitendo cha wakandarasi kutokuwepo katika maeneo yao ya kazi na kutohudhuria kikao kama ilivyoagizwa kinakwamisha utekelezaji wa miradi na hivyo kuutaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kujulisha kampuni husika kuandika maelezo ya kutokuwepo kwenye maeneo ya kazi na kukwamisha juhudi za Serikali katika usambazaji wa umeme vijijini.
“ Kama Serikali tumeweka mikakati ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2019- 2021 vijiji vyote nchini vinafikiwa na huduma ya umeme, sasa inapotokea baadhi ya wakandarasi wanakwamisha juhudi hizi wakati wamekwishalipwa na Serikali ni lazima Serikali iwawajibishe kulingana na sheria na kanuni za nchi,” alisema Mgalu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifafanua jambo mbele ya wanakijiji wa kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na serikali wakisikiliza kero mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wanakijiji wa kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto mbele) akiendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifafanua jambo kwa wakazi wa kijiji cha Magumbani kilichopo wilayani Mkinga mkoani Tanga.
Hivyo makala Naibu Waziri Mgalu Awataka Wakandarasi Tanga kutoa Maelezo Ya kutokuanza Miradi
yaani makala yote Naibu Waziri Mgalu Awataka Wakandarasi Tanga kutoa Maelezo Ya kutokuanza Miradi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Mgalu Awataka Wakandarasi Tanga kutoa Maelezo Ya kutokuanza Miradi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/naibu-waziri-mgalu-awataka-wakandarasi.html
0 Response to "Naibu Waziri Mgalu Awataka Wakandarasi Tanga kutoa Maelezo Ya kutokuanza Miradi"
Post a Comment