title : MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA
kiungo : MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA
MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA
Waziri
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina ameridhia maamuzi ya Kampuni ya Ranchi za NARCO kuvunja
mkataba baina ya mwekezaji Agri Vision Global Ltd na serikali katika Ranchi ya Kagoma mkoani Kagera na kuamuru aondoka mara moja
baada ya mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba huo katika kipindi cha
miaka mitano.
Waziri
Mpina ametoa maelekezo hayo jana alipotembelea Ranchi ya Kagoma kuangalia
shughuli mbalimbali katika Ranchi hiyo
ambapo ametoa siku saba kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo na badala
yake Serikali kupitia NARCO kuendelea kusimamia shughuli za mifugo katika
Ranchi hiyo.
“Ninakuagiza Mkuu wa Wilaya kuanzia sasa
hakikisha unaimarisha ulinzi katika ranchi hii katika kipindi cha
kukabidhi Ranchi baina ya Serikali na Mwekezaji
ili kusitokee hujuma zozote” alisisitiza Mpina
Alitaja
baadhi ya mambo ambayo hayakutekelezwa na mwekezaji huyo kuwa ni pamoja na kujenga
machinjio ya nyama, kujenga
kiwanda, kutoa gawio la shilingi bilioni tatu kila mwaka katika kipindi cha
miaka mitano, kutoa shilingi 2672 kwa hekta moja kama tozo la ardhi na
kushindwa kuendeleza miundombinu ya NARCO waliyoikuta wakati wanaingia mikataba hiyo miaka mitano
iliyopita.
Waziri
Mpina amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO,
Profesa Philemoni Wambura kuhakikisha kwamba ndani ya siku saba
anamleta Meneja katika Ranchi hiyo kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za ranchi
hiyo na kuhakikisha kuwa inafanya kazi zake kisasa.
Aidha
Mpina ametoa siku saba kwa Uongozi wa NARCO kuhakikisha kuwa imefanya
tathmini ya hasara zilizosababishwa na
mwekezaji huyo ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi yake ili aweze kuilipa Serikali ikiwa ni pamoja na
shilingi bilioni kumi na tano kama gawio
la miaka mitano iliyokaa ambalo amesema halijawahi kulipwa hata shilingi moja.
“Sasa
tumeamua kuchukua hatua na tutaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wawekezaji
wasiowaaminifu wanaotaka kuihujumu serikali katika sekta hizi za mifugo na
Uvuvi” alihoji Mpina
Alionya
wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kwamba wanauwezo wa kuwekeza
katika vitalu ili wapewe lakini wanabadili
matumizi baada ya kupewa. Aliongeza kwamba
Serikali imegundua baadhi ya
wawekezaji wanaopewa vitalu wanawakodisha wafugaji kutoka nchi jirani na kujipatia faida wakati Serikali haipati chochote.
Hivyo makala MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA
yaani makala yote MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/mpina-abariki-narco-kuvunja-mkataba-wa_6.html
0 Response to "MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA"
Post a Comment