title : MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO
kiungo : MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO
MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde amefanya ziara kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata ya Hombolo Bwawani huku akiwahakikishia wananchi wa Mkoyo kuwa wataanza kupata huduma ya maji safi na salama kabla ya mwaka mpya kutokana na mradi huo kukamilika kwa asilimia 95.
Mavunde amefanya ziara hiyo jana ambapo ametembelea kata hiyo na kufanya mikutano ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi, ambapo akiwa kijiji cha Mkoyo miongoni mwa kero walizolalamikia wananchi ni utekelezaji wa mradi ya maji.Kutokana na malalamiko hayo, Mavunde amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 95 lakini bado kuna mapungufu machache ambayo mkandarasi anatakiwa kurekebisha na kuukabidhi kwa wananchi ili waweze kupata maji safi na salama kabla ya mwaka mpya.
Kwa upande wa sekta ya Elimu, Mbunge huyo ameahidi kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa shule mbili za msingi kwenye eneo la Ngh’ole na Ndachi kutokana na watoto wa wanatembea umbali mrefu kufuata elimu.“Hivyo kwa kuanza tunaanza na nguvu ya wananchi kwenye ujenzi wa shule ambapo kwa upande wangu nitachangia matofali 1000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili kuanza harakati za ujenzi wa shule hizi,”amesema
Akiwa katika mtaa wa Hombolo bwawani,Mavunde ameahidi kununua mota yenye thamani ya Tsh 4,000,000 na kuwafungia wananchi ili waanze kupata maji kwenye Mradi wa Maji wa Mtaa wa Bwawani B ambao mota yake imekufa.
Aidha katika Mradi mkubwa wa Maji wa Hombolo ambao ulihujumiwa kwa kuibiwa solar panel,Mavunde amesema wamefanikiwa kuwakamata wezi waliohujumu mradi huo na taratibu za kipolisi zinafanywa ili vifaa hivyo virejeshwe Hombolo na wananchi waanze kupata maji.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kata ya Hombolo Bwawani.
Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani Assedi Ndajilo akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde wa kusikiliza kero za wananchi.
Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa hadhara kata ya Hombolo bwawani
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi na viongozi wa kata ya Hombolo bwawani.
Hivyo makala MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO
yaani makala yote MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/mavunde-ajibu-kero-za-wananchi-wa.html
0 Response to "MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO"
Post a Comment