MAASKOFU WATOA YA MOYONI.

MAASKOFU WATOA YA MOYONI. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAASKOFU WATOA YA MOYONI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAASKOFU WATOA YA MOYONI.
kiungo : MAASKOFU WATOA YA MOYONI.

soma pia


MAASKOFU WATOA YA MOYONI.


Mwambawahabari

MAASKOFU mbalimbali nchini wameitumia Sikukuu ya Krismasi kuelezea mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.


Huku baadhi yao wakimpongeza Rais,Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuachia baadhi ya wafungwa waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa na wale wa vifungo vya maisha jela.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustine Shao, amempongeza Rais kuwaachia huru wafungwa hao kwani inaonesha wazi anaamini waliopo magerezani wakiwemo vijana wataendelea kujirekebisha na kuwa na tabia njema inayompendeza Mungu na jamii nzima.

Pia amewataka waumini wa Kikristo kujitakasa upya hasa katika Sikukuu ya Krismasi . “Ni vema pia Watanzania kila mmoja wetu akaheshimu mawazo ya mwenzake hata kama yanatofautiana”.

Askofu Pengo ahimiza mema


Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesisitiza umuhimu wa Watanzania kutenda matendo mema na kuongozwa na hofu ya Mungu.


Askofu Pengo amesema hayo kwenye Misa ya pili ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo iliyofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.


Amesema maendeleo hayawezi kuja kama Watanzania wenyewe hawana maadili au hofu ya Mungu.“Kila mmoja wetu awe mwananchi au kiongozi, anapaswa kuwa na hofu ya Mungu itakayomuongoza katika kufanikisha mipango iliyokusudiwa au aliyoikusudia.


“Pia Watanzania wanapaswa kukubali kuongozwa na kuwaombea viongozi wao ili jitihada zinazofanywa zizae matunda mema kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake,” amesema Askofu Pengo


ASKOFU Amani azungumzia utekaji nyara

Wakati huo huo Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi, mkoani Kilimanjaro Isack Amani, amekemea vitendo vya ukatili vikiwamo vya utekaji nyara na mauaji ya kinyama yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini.

Amesema matukio hayo yanatishia kutoweka kwa amani iliyopiganiwa na waasisi wa Taifa kwa miaka mingi.


Akihubiri kwenye ibada ya Krismasi iliyofanyika Kanisa Kuu la Kristu Mfalme Moshi, Askofu Amani alisema katika kipindi cha muda mfupi kumeibuka matukio yanayohatarisha amani ya nchi yetu.

Na Said Mwishehe,Blogu ya Jamii


Hivyo makala MAASKOFU WATOA YA MOYONI.

yaani makala yote MAASKOFU WATOA YA MOYONI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAASKOFU WATOA YA MOYONI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/maaskofu-watoa-ya-moyoni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAASKOFU WATOA YA MOYONI."

Post a Comment