title : Lukuvi Mgeni Rasmi mkutano wa Wataalam wa Ardhi Morogoro
kiungo : Lukuvi Mgeni Rasmi mkutano wa Wataalam wa Ardhi Morogoro
Lukuvi Mgeni Rasmi mkutano wa Wataalam wa Ardhi Morogoro
Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam LUKUVI anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa mwaka wa Wataalam wa Ardhi wa Wataalam wa Ardhi waliowai kusoma Chuo cha Ardhi Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Wataalam Waliowai kusoma Cha Ardhi Morogoro, Salum Shaka ,alisema mkutano huo unatarajia kufanyika machi 2018 lengo la mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano ya Umoja huo ambayo inafanyika kila mwaka.
"Umoja wa Wataalam wa Chuo cha Ardhi Morogoro tumeweka utaratibu kila mwisho wa mwaka kufanya tathimini na kujadili Maendeleo ya Umoja wetu " alisema Shaka.
Salum alisema kongamano hilo mwaka huu linatarajia kupambwa na WAZIRI mwenye dhamana Wiriam LUKUVI katika viwanja vya vya Chuo hicho .
Aliwataka wataalam wote ambao waliwai kusoma Chuo hicho wajitokeze siku hiyo kuzungumza na WAZIRI wao katika viwanja vya Chuo.
" Siku hii ni maalum kwetu ambapo mwanzoni mwa machi 2018 tutakutana mambo mbali mbali ya Chuo yatajadiliwa kwa lengo la kupanua wigo wataalam kwa wataalam kujenga uwezo katika utendaji wa majukumu yao na kujenga weledi wakiwa kazini" alisema.
Alisema siku hiyo ni maalum kwa kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya ardhi.
Aidha alisema kwa sasa nchi yetu inaelekea Tanzania ya Viwanda na kauli mbiu siku hiyo" Ardhi ni msingi Mkuu kufikia azima ya Tanzania ya Viwanda"
Mwisho
Hivyo makala Lukuvi Mgeni Rasmi mkutano wa Wataalam wa Ardhi Morogoro
yaani makala yote Lukuvi Mgeni Rasmi mkutano wa Wataalam wa Ardhi Morogoro Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Lukuvi Mgeni Rasmi mkutano wa Wataalam wa Ardhi Morogoro mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/lukuvi-mgeni-rasmi-mkutano-wa-wataalam.html
0 Response to "Lukuvi Mgeni Rasmi mkutano wa Wataalam wa Ardhi Morogoro"
Post a Comment