title : DOKTA MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA NORWAY
kiungo : DOKTA MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA NORWAY
DOKTA MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA NORWAY
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway hapa nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad na kutoa wito kwa wawekezaji kutoka Norway kuja kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo Nishati, misitu, kilimo, gesi na mafuta.
Dkt. Mpango amemweleza Balozi huyo kwamba Tanzania iko katika hatua mbalimbali za kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda na kwamba wawekezaji kutoka Norway watakuwa na mchango mkubwa wa kuiwezesha Tanzania kufikia lengo hilo.
Aliyataja maeneo ya kuongeza thamani ya mazao ya misitu, mifugo, uvuvi, nishati, kilimo na mengine mengi kwamba yataongeza tija katika sekta hiyo na kwamba malighafi za kilimo zitatochea uzalishaji katika viwanda na kuinua kipato cha wananchi.
“Tumeamua kujenga Reli ya Kati kwa viwango vya kimataifa-SGR ambayo inahitaji umeme wa kutosha kwa hiyo bado tunahitaji mchango wa wadau mbalimbali ikiwemo Norway ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na nishati ya umeme ya kutosha na ya uhakika ili kufanikisha mradi huo mkubwa” aliongeza Dkt. Mpango
Kuhusu Sekta Binafsi, Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali imeendelea na majadiliano na Sekta hiyo ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwemo masuala ya kodi pamoja na kujenga kuaminiana kati ya pande hizo mbili.Amefafanua kuwa Sekta Binafsi ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa na kwamba vikao hivyo vya mara kwa mara vimeanza kuzaa matunda.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (hayupo pichani) mjini Dodoma.
Katibu wa Waziri wa Fedha na Mipango Bw. Edwin Makamba (kushoto) na Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Idara ya Fedha za Nje Bw. Anayeshughulikia dawati la Norway Bw. Warioba Nyakua, wakifuatilia majadiliano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na mgeni wake, Balozi wa Norway hapa nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiteta jambo na Kamishna wa Bajeti wa Wizara hiyo Bi. Mary Maganga (kushoto) na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. John Rubuga, wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (hayupo pichani) mjini Dodoma.
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) akizungumza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) mjini Dodoma. Kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje-Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga.
Hivyo makala DOKTA MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA NORWAY
yaani makala yote DOKTA MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA NORWAY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DOKTA MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA NORWAY mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/dokta-mpango-aalika-wawekezaji-kutoka.html
0 Response to "DOKTA MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA NORWAY"
Post a Comment