Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine

Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine
kiungo : Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine

soma pia


Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine

MWANAMUME mwenye umri wa miaka 21 alijitia kitanzi kwa mti katika msitu wa KCC ulio wadi wa Bidii, mjini Kitale baada ya kugombana na mpenzi wake kuhusu mwanamume mwingine aliyekutana naye katika tumbuizo la muziki.


Ilidaiwa Bw Gideon Simiyu, alihudhuria tamasha ya mwanamuziki kutoka Uganda, Jose Chameleon, katika kilabu cha Epic mkesha wa Krismasi akiwa na mpenzi wake.

Alikasiirishwa wakati mpenzi wake ambaye bado hajatambuliwa, alipoamua kusakata densi na mwanamume mwingine kilabuni ndipo akajitia kitanzi Jumatano.


Kulingana na Bw Isaac Wafula, ambaye ni binamu yake anayeishi kijiji cha Matisi, marehemu alionekana mara ya mwisho katika soko la Matisi mnamo Jumapili usiku akipigana na mpenzi wake walipokuwa wakirudi nyumbani.
“Alikuwa mwenye hasira sana aliporudi nyumbani. Aliniambia waligombana na mpenzi wake kwa sababu ya mwanamume ambaye mpenzi wake alikutana naye na kucheza densi pamoja kilabuni. Baadaye alienda moja kwa moja hadi chumbani mwake kisha akaondoka bila simu yake,” akasema Bw Wafula.
Aliongeza kuwa katika siku ya Krismasi, marehemu aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kwamba wengi watamtamani ifikapo mwaka wa 2018.
Aliandika jumbe mbili kwenye mtandao huo kusema: “2018 nitaiona kweli? Mungu nisaidie.”
Mwingine ukasema: “Wallahi naona nikibaki 2017.”
Bw Dickinson Chelee, ambaye ni bawabu, alisema mwili wa marehemu ulionekana ukining’inia mtini ukiwa na kamba shingoni mwake.
Mkuu wa polisi wa Trans Nzoia, Bw Jackson Mwenga, alithibitisha kisa hicho na kusema upelelezi umeanzishwa.
“Tulitembelea eneo la mkasa tukapata mwili wa marehemu Gideon Simiyu, ukining’inia mtini. Tunashuku alijitoa uhai lakini tumeanzisha uchunguzi,” akasema.
Mwili huo ulipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kitale ukisubiri kufanyiwa upasuaji kubainisha chanzo halisi cha kifo.


Hivyo makala Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine

yaani makala yote Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/ajiua-baada-ya-mpenzi-wake-kucheza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Ajiua Baada ya mpenzi wake kucheza Muziki na Mwanaume mwingine"

Post a Comment