AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde

AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde
kiungo : AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde

soma pia


AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye Makao yake makuu jijini Arusha inafanya ziara ya kikazi katika Jamhuri ya Cape Verde ili kukutana na kuelimisha wadau mbalimbali nchini humo kwa lengo la kuiitangaza Mahakama hiyo.

Uelimishaji huo ni miongoni mwa juhudi zinazofanyika na Mahakama hiyo ili kuongeza uelewa wa wadau husika kuhusu jukumu na ujumbe wa AFCHPR katika suala zima la kulinda haki za Binadamu baranni Afrika na pia kuzihimiza nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuridhia itifaki iliyounda Mahakama hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 34(6) na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali Mamlaka ya AfCHPR kupokea kesi za Watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali.

Katika ziara hiyo ya siku tatu inayoanza leo,13/12/2017 Jumatano wajumbe wake ambao ni pamoja na Majaji watatu na baadhi ya maofisa wa ofisi ya Msajili wa Mahakama hiyo watakutana na Rais wa Cape Verde,Waziri mkuu na Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo na wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria na wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali.

Rais wa Mahakama hiyo ya Afrika ya haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Ore’ alisema ziara hiyo ya uelemishaji kuhusu Mahakama hiyo ni wan ne kufanyika kwa mwaka huu na kwamba juhudi hizo zitaendelea mwaka ujao wa 2018.

“Ili kufanikisha malengo ya AfCHPR na pia kuimarisha mfumo wa Haki za Binadamu barani Afrika nchi za umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa mujibu wa kifungu husika” alisema Jaji Ore’.

Tayari kwa mwaka huu uelimishaji huo umefnayika katika nchi za Jamhuri ya kiarabu ya Misri,Tunisia na Guinea Bissau.

Aidha hadi sasa ni nchi 30 tu kati ya 55 wanachama wa umoja wa Afrika ikiwemo Tanzania ndiyo zimeridhia itifaki iliyoanzisha AfCHPR na kati ya hizo ni nchi 8 tu ndiyo zimekwisha toa tamko la kuitambua Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.


Hivyo makala AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde

yaani makala yote AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/afchpr-ziarani-jamhuri-ya-cape-verde.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde"

Post a Comment