title : WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
kiungo : WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
Serikali imewataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kurejesha ari na hamasa ya jamii kushiriki katika kazi za maendeleo ili kutoa mchango katika kufikia Tanzania ya Viwanda na yenye uchumi wa kati.
Kauli hii imetolewa MJini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 12 wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unafoanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa kupitia Mkutano huo Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wanatakiwa kutoa mapendekezo kuhusu mbinu bora zitakazosaidia kurudisha ari na hamasa ya jamii kushiriki katika maendeleo na hivyo kusaidia kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.
Mhe. Ummy Mwalimu amefafanua kuwa wataalam wa maendeleo ya jamii ndiyo wenye jukumu la kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya kisekta hususan kilimo, afya, elimu, na miundo mbinu na kadhalika.
“Wataalam wa Maendeleo ya Jamii watumie fursa hii kujitathmini ili kupata majibu ya namna bora ya kutekeleza majukumu yao ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki kwenye uzalishaji na kutokomeza ukatili wa jinsia ambao unapunguza kasi ya kufikia uchumi wa kati na maendeleo jumuishi” alisema Mhe. Ummy.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb) akisisitiza maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo kuelekea uchumi wa Viwanda wakati akifungua Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Mandeleo ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akitambulisha washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2017 unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma na kujumuisha Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Taifa, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Mitaa na wawakilishi kutoka Sekta na Mashirika mbalimbali nchini.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Elimu Bw. Tikson Nzunda akifafanua neno wakati wa Mkutano MKuu wa Kitaifa wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2017 unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma kuhusu umuhimu wa kuwatumia wataalamu wa Maendeleo ya Jamii katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo yao.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akitambulisha malengo ya Mkutano Mkuu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii 2017 na kumkaribisha Mgeni rasmi Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii
Baadhi ya Maaafisa Maendeleo ya Jamii wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb)(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini unaofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
Hivyo makala WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
yaani makala yote WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/waziri-ummy-awataka-maafisa-maendeleo.html
0 Response to "WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO"
Post a Comment