WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA.

WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA.
kiungo : WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA.

soma pia


WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA.

Na John Nditi, Kilimbero

WAZIRI wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amesema kuwa suala ya kupanua viwanda vya sukari nchini halina mbadala ni jambo la lazima ili kukidhi uchakataji mkubwa wa miwa inayolimwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa sukari na ya bei nafuu.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na Menejimenti ya Kiwanda cha Sukari Kilombero kiwandani hapo pamoja na kwa baadhi ya wakulima na viongozi wa vyama vya zao la miwa wa pande mbili za wilaya ya Kilosa na Kilombero kwenye ukumbi wa Chuo cha Sukari Kilombero.

Alisema ,Serikali ilipoamua kuuza sehemu ya hisa zake kwa kampuni binafsi , lengo lake lilikuwa ni moja kwamba wanauowezo wa kifedha unaoendana na ufanisi na upanuzi wa viwanda kuweza kukidhi mahitaji ya zao la miwa na utengeenzaji wa sukari.

Dk Tizeba alisema , kutokana na dhana hiyo, maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuona viwanda vya sukari vinapanuliwa kwa ajili ya kukidhi usagaji wa miwa nayolimwa na mashamba ya viwanda nay a wakulima wan je na kutengeneza sukari nyingi za kujitoshereza.

Alisema ,uamuzi hyo unatokana na kubaini kuwa viwanda uwezo vya sukari ni mdogo kuchakata tani nyingi za miwa kwa msimu wa kilimo ikiwemo miwa ya wakulima wa n je na badala yake kusalia shambani na kuharibika.

“ Kinachohitajika ni utosherezaji wa sukari nchini na ya bei nafuu ,kama uwezo wa viwanda ni mdogo kuchakata miwa na kuzalisha sukari kinachohitajika ni upanuzi wa kiwanda ” alisema Dk Tizeba.Dk Tizeba alisema, kinachofanyika kwa sasa ni kuweka programu ya wizara na wenye viwanda kutakiwa kuwasilisha mpango kazi wao unaoinesha hatua za utekelezaji wa upanuzi wa viwanda vyao kikiwemo cha Kilombero .

Naye Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe, alimwomba Waziri kuuangalia kwa karibu zaidi mkoa huo kwani utafiti wake umeonesha ni kitovu cha kuzalisha sukari nchini na maziwa makuu kwa kufikisha zaidi ya tani milioni moja za sukari .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero, Guy Willium akitoa maelezo ya uendeshaji na uzalishaji wa sukari katika kikao na Waziri , licha ya kueleza faida na changamoto zinazokikabili alisema ,zinahitajika zaidi ya Sh bilioni 500 kwa ajili ya mpango endelevu wa upanuzi kiwanda .Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema , mpango huo utatekelezwa kwa awamu nay a kwanza ya miaka minne kulingana na upatikanaji wa fedha ikamilika kufikia June 2021 na kukamilishwa hadi ifikapo mwaka 2025.

Alisema ,kutokana na mpango wa upanuzi wa kiwanda na mashamba ya miwa , uzalishaji wa sukari utaongezeka kutoka wastani wa tani 125,000 kwa mwaka zinazozalishwa hadi kufikia wastani tani za sukari 260,000 kwa mwaka.
Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba ( kati kati) akijadiliana na Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ( kushoto) alipofanya ziara ya kikazi katika Kiwanda kilichopo sehemu ya wilaya mbili ya Kilombero na Kilosa, mkoani Morogoro kwa ajili ya kuona shughuli za uzalishaji wa sukari na kilimo cha zao la miwa kwa kiwanda na wakulima wa nje
Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero, Guy Willium , wakati alipofanya ziara katika Kiwanda kilichopo sehemu ya wilaya mbili ya Kilombero na Kilosa, mkoani Morogoro kwa ajili ya kuona shughuli za uzalishaji wa sukari na kilimo cha zao la miwa kwa kiwanda na wakulima wa nje.

Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba akiteremka kutoka katika ndege ndogo baada ya yeye na viongozi wengine wa mkoa , wilaya za Kilombero na Kilosa , Bodi ya Sukari na wataalamu wa Kilimo kukagua eneo la mashamba makubwa ya miwa waliyolimwa na kupanuliwa na Kiwanda cha Sukari Kilombero waiiwa angani mara baada ya kupatiwa taarifa ya Kiwanda hicho na Mkurugenzi Mtendaji Guy Willium , wakati alipofanya ziara kwa ajili ya kuona shughuli za uzalishaji wa sukari na kilimo cha zao la miwa kwa kiwanda na wakulima wan je. ( Picha na John Nditi).


Hivyo makala WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA.

yaani makala yote WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/waziri-ataka-utekelezaji-upanuzi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA."

Post a Comment