title : WATOTO 20 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA
kiungo : WATOTO 20 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA
WATOTO 20 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) ya nchini Israel wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa watoto 20 wenye matatizo ya Moyo.
Upasuaji huo ambao unatumia mtambo wa Cathlab umefanyika katika kambi maalum ya matibabu iliyoanza tarehe 23/11/2017 na kumalizika kesho tarehe 27/11/2017. Matibabu yaliyofanyika ni ya kuziba matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo.
Katika kambi hii tunatarajia kufanya uchunguzi wa moyo kwa watoto 100 kati ya hao watoto 60 ambao watakuwa na matatizo makubwa watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua mwakani na watoto 40 watatibiwa hapa nchini.
Tumepanga kufanya matibabu kwa watoto 25 tunaamini hadi kambi itakapomalizika watoto wote hawa watakuwa wamepata matibabu. Watoto 20 waliopata matibabu wengine wameruhusiwa na waliobaki hali zao zinaendelea vizuri na wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika.
Tangu mwaka 2015 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ilianza kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart- SACH) ya nchini Israel ambapo hadi sasa jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel. Gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na Taasisi hii.
Tunawashukuru sana wenzetu hawa wa SACH kwa kuona umuhimu wa kutoa huduma ya matibabu bure kwa watoto wenye matatizo ya moyo. Watoto waliotibiwa wamepona na wale ambao walikuwa wanafunzi wanaendelea na masomo yao.
Hivyo makala WATOTO 20 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA
yaani makala yote WATOTO 20 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATOTO 20 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/watoto-20-wenye-matatizo-ya-moyo.html
0 Response to "WATOTO 20 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA"
Post a Comment