title : WATANZANIA WAISHIO CHINA WATAKIWA KUCHANGIA JUHUDI ZA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA
kiungo : WATANZANIA WAISHIO CHINA WATAKIWA KUCHANGIA JUHUDI ZA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA
WATANZANIA WAISHIO CHINA WATAKIWA KUCHANGIA JUHUDI ZA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA
Na Happiness Shayo- China.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe Mbelwa Kairuki amewataka Watanzania wanaosoma katika Taifa hilo kutumia fursa hiyo kuunga mkono juhudi za Tanzania kuelekea Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa shirikisho la Jumuiya za Watanzania wanaosoma katika Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Wuhan, Jimbo la Hubei.
Balozi Kairuki alisema kuwa yapo maeneo kadhaa ambayo Watanzania hao wanaweza kutoa michango yao katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwenye ujenzi wa Viwanda ili sekta hiyo isaidie na kuleta tija katika ukuaji wa Uchumi.
Akizungumzia kuhusu sekta ya Utalii, Balozi Kairuki aliitaja China kama soko jipya wanalopatikana watalii na kwamba kwa mwaka 2016 ni Wachina Millioni 120 waliokwenda nje ya nchi kutalii sawa na idadi ya watu wote wa nchi za Tanzania,Kenya,Uganda,Burundi na Rwanda, idadi inayoonekana ni kubwa sana,ambapo kwa mwaka huo huo ni watalii 30,000 walipokelewa Tanzania kutoka China.
“Zipo hatua kadhaa ambazo sasa zimechukuliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini China, hivi sasa tunazungumza na kampuni kubwa inayomiliki mitandao ya kijamii hapa ya China ya TENCENT ili tuweze kutumia mtandao wao wa QQ kurusha vivutio vyetu vya utalii hapa China mubashara, lakini pia mwezi huu tulikuwa na Mazungumzo na Serikali ya China kuwajulisha nia ya shirika letu la ndege la Air Tanzania kuanza safari za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Guangzhou.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akihutubia katika mkutano wa Shirikisho la Jumuiya ya Watanzania wanaosoma katika Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Watanzania wanaosoma nchini China (TASAFIC) Bw. Remidius Emmanuel akizungumza katika mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni.
Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China (Mwambata wa Elimu) Bw. Lusekelo Gwassa Akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa TASAFIC kwa Mwaka 2017.
Baadhi ya Watanzania wanaosoma nchini China waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya ya Watanzania wanaosoma katika Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni.
Baadhi ya Watanzania waliohudhuria Mkutano Mkuu wakiwa katika Picha ya pamoja na Balozi Mbelwa Kairuki.
Hivyo makala WATANZANIA WAISHIO CHINA WATAKIWA KUCHANGIA JUHUDI ZA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA
yaani makala yote WATANZANIA WAISHIO CHINA WATAKIWA KUCHANGIA JUHUDI ZA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAISHIO CHINA WATAKIWA KUCHANGIA JUHUDI ZA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/watanzania-waishio-china-watakiwa_2.html
0 Response to "WATANZANIA WAISHIO CHINA WATAKIWA KUCHANGIA JUHUDI ZA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA"
Post a Comment