Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha

Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha
kiungo : Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha

soma pia


Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha

Na Mwandishi Wetu

WAHITIMU wa Shule kongwe ya Sekondari Ndanda iliyopo Masasi mkoani Mtwara, kupitia umoja wao (UWAHISSENDA) wanakusudia kuanzisha kampuni itakayotoa mikopo midogomidogo kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi. Hatua hiyo imekuja miaka miwili baada ya wahitimu hao kuanzisha kundi la mtandao wa kijamii la Whatsaap lenye zaidi ya wanaumoja 250, na hivyo hivi karibuni kuazimia pamoja na kuimarisha umoja wao, wafikirie pia kuinuana kiuchumi.

Akizungumza baada ya kikao cha wanaumoja hao hivi karibuni, Kaimu Mwenyekiti wa UWAHISSENDA, Yohana Kasawala alisema dhamira yao itaanza kutekelezwa mapema mwakani baada ya kuwa tayari wameshapata mtaji kutokana na michango ya wanachama. Alisema, pamoja na kukopeshana huku riba ikitumika kutunisha mfuko wa umoja, wanakusudia kutanua wigo wa mikopo hata kwa wasio wanaumoja wa UWAHISSENDA.

Aidha, mipango hiyo ya kuinuana kiuchumi inakwenda sambamba na mpango wa uzinduzi wa umoja huo uliopangwa kufanyika shuleni Ndanda mapema mwakani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo. “Daima umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu, nasi tumeona ni vyema tukatumia mshikamano huu kama fursa ya kujiimarisha kiuchumi. Tuna ndoto nyingi, lakini kwa kuanzia tunakuja na hili la kampuni ya mikopo midogomidogo yaani Microfince company…

“Wataalamu wetu wa uchumi ndani ya umoja ambao wametapakaa katika taasisi za fedha nchini wametupatia mchanganuo wenye kutia matumaini kwamba tutaweza, na kama mambo yatakwenda hivyo, siku za usoni tunaweza kufikiria hata kuanzisha benki…Ni suala la muda tu,” alisema Kasawala na kuongeza kuwa, umoja una Katiba, umesajiliwa kisheria na kufuata taratibu nyingine za nchi.

Ndanda, shule iliyoanzishwa mwaka 1928, ni miongoni mwa shule kongwe zilizotoa wasomi wengi waliobahatika kushika nyadhifa mbalimbali katika nchi, miongoni mwao akiwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Pia wamo Hawa Ghasia, mmoja wa mawaziri waandamizi katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Nishati katika Serikali ya Rais, Dk John Magufuli pia ni matunda ya sekondari ya Ndanda.


Hivyo makala Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha

yaani makala yote Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/wahitimu-ndanda-kuanzisha-kampuni-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wahitimu Ndanda kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha"

Post a Comment