title : UMOJA WA ULAYA WAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 130 KUSAIDIA UPATIKANAJI UMEME VIJIJINI
kiungo : UMOJA WA ULAYA WAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 130 KUSAIDIA UPATIKANAJI UMEME VIJIJINI
UMOJA WA ULAYA WAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 130 KUSAIDIA UPATIKANAJI UMEME VIJIJINI
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
TANZANIA imezidi kupata neema kutoka Jumuiya ya Kimataifa ambapo Novemba 2, 2017, Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 50, takriban Shilingi bilioni 130 kwa ajili ya kufadhili Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini unaoendeshwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Mkataba wa Makubaliano hayo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Neven Mimica.
Msaada huo umelenga kuwasaidia raia wa Tanzania kufikiwa na huduma nafuu ya nishati ya umeme kwa kupanua uwezo wa gridi ya Taifa pamoja na mtandao wa usambazaji umeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa msaada huo mkubwa utakaoiwezesha nchi kuwa na umeme wa uhakika utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu wake.“Umoja wa ulaya ni wadau wetu muhimu wa maendeleo kutokana na misaada muhimu na mikubwa wanayotupatia, na kusadia agenda yetu ya maendeleo” alisema Bw. James
Alisema kuwa kiasi cha msaada wa Euro milioni 50 kilichotolewa na Umoja huo bila masharti yoyote si kidogo, na kwamba kitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme utakaochangia kuimarika kwa sekta ya viwanda itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza kwa makini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akitoa maelezo ya ujio wa ugeni huo kuwa ni neema kwa nchi ya Tanzania kwani Umoja wa Ulaya wametoa msaada wa Euro Milioni 50 utasaidia vijijini 3600 nchini kupata umeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) na akimweleza jambo Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Mr. Neven Mimica wakati wa hafla fupi ya Umoja wa Ulaya (EU) kutiliana saini makubaliano ya msaada wa Euro milioni 50 kwa ajili ya kusaidia usambazi wa umeme vijijini kupitia Mradi Kabambe wa Kusambaza umeme Vijijini (REA).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiwa pamoja na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Bw. Neven Mimica wakisaini Mkataba wa msaada wa fedha za kusaidia usambazaji wa umeme Vijijini (EURO milioni 50) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Mr. Neven Mimica, wakibadilishana hati za makubaliano ya msaada wa ruzuku ya kiasi cha EURO Milioni 50 katika ukumbi wa wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UMOJA WA ULAYA WAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 130 KUSAIDIA UPATIKANAJI UMEME VIJIJINI
yaani makala yote UMOJA WA ULAYA WAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 130 KUSAIDIA UPATIKANAJI UMEME VIJIJINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UMOJA WA ULAYA WAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 130 KUSAIDIA UPATIKANAJI UMEME VIJIJINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/umoja-wa-ulaya-waipatia-tanzania-msaada.html
0 Response to "UMOJA WA ULAYA WAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 130 KUSAIDIA UPATIKANAJI UMEME VIJIJINI"
Post a Comment