title : TUPAMBANE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA: WAZIRI KAIRUKI.
kiungo : TUPAMBANE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA: WAZIRI KAIRUKI.
TUPAMBANE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA: WAZIRI KAIRUKI.
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Watanzania wametakiwa kutumia nguvu zao katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.
Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa kimsingi kiwango cha ukatili wa kijinsia nchini na dunia bado ni kubwa na kwa mujibu wa Taarifa ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2015/2016 inaonesha kuwa wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.
Ameongeza kuwa takwimu zinonesha kuwa asilimia 42 ya wanawake waliowahi kuolewa wamekumbana na ukatili wa wenza wao ama wa kimwili,au ukatili unaohusisha ngono.“Nawaomba watanzania wenzangu katika maeneo yenu pazeni sauti na kufanya kwa vitendo kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia unaowakumba sana wanawake na watoto” alisema Mhe. Angellah.
Aidha kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa athari za ukatili wa kijinsia ni kubwa sana katika Nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akinyajua bango juu lenye ujumbe unaosema “Ukatili wa Kijinsia Unachelewesha Tanzania ya Viwanda” wakati akipokea Maandamano maalum ya ufunguzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Baadhi ya wananchi na wadau wa maendeleo wakiwa katika maandamano maalum ya ufunguzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akiwaasa wadau na watanzania kujikita katika kupambana na ukatili wa kijinsia wakati akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.
Niabu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akieleza namna Wizara inavyoshikiana na wadau na wananchi kupambana kuondoa ukatili wa kijinsia katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.
Mkurugenzi wa Shirika la WILDAF Tanzania Dkt Judith Odunga akitoa salamu kwa niaba ya wadau katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leade’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TUPAMBANE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA: WAZIRI KAIRUKI.
yaani makala yote TUPAMBANE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA: WAZIRI KAIRUKI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUPAMBANE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA: WAZIRI KAIRUKI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/tupambane-kupinga-ukatili-wa-kijinsia.html
0 Response to "TUPAMBANE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA: WAZIRI KAIRUKI."
Post a Comment