Serikali Yaishukuru China

Serikali Yaishukuru China - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali Yaishukuru China, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali Yaishukuru China
kiungo : Serikali Yaishukuru China

soma pia


Serikali Yaishukuru China


Na Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amemshukuru Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke kwa kuipatia wizara vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 133.

Waziri Dkt. Mwakyembe ametoa shukrani hiyo leo Ofisini kwake Mkoani Dodoma alipokutana na Balozi huyo ambapo waliweka sahihi ya makabidhiano ya vifaa hivyo na kuhaidi kuendelea kuimarisha uhusiano huo uliodumu kwa muda mrefu .

“Nashukuru sana Balozi kwa kutupatia msaada wa vitendea kazi na tunaahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili kwa manufaa ya taifa na watu wake” amesema Mhe.Dkt. Mwakyembe.

Aidha Waziri Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa tayari kumekuwa na juhudi za wazi zinafofanywa na Ubalozi huo kwa kutoa mafunzo ya kubadilishana utaalam kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa china kupitia sekta za filamu, habari,michezo na utamaduni.

Pia, Dkt. Mwakyembe alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania imepata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika wenye lengo ya kuhifadhi kumbukumbu za harakati za kuikomboa Afrika ili kuwa na historia nzuri kwa kizazi kijacho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke (Kulia) katika ofisi za Wizara leo Mkoani Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke (Kulia) wakiweka saini makubaliano ya kukabidhiana vifaa vya ofisi vyenye thamani ya shilingi milioni 133 katika ofisi za Wizara leo Mkoani  Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke (wa pili kulia) pamoja na watendaji wa Wizara leo Mkoani Dodoma.Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,DODOMA.



Hivyo makala Serikali Yaishukuru China

yaani makala yote Serikali Yaishukuru China Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Yaishukuru China mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/serikali-yaishukuru-china.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Serikali Yaishukuru China"

Post a Comment