RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi

RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi
kiungo : RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi

soma pia


RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo amewaasa watumishi wa mashirika ya umma na wakala wa serikali mkoani Rukwa kutotumia vyeo vyao kuwanyanyasa wananchi wanaowahudumia na badala yake wawasaidie kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa bila ya kujali, rangi kabila, dini na hali zao kiuchumi.

Amesema kuwa watumishi wa serikali ni watumishi wa wananchi hivyo wanapaswa kujituma bila ya kujali vyeo vyao kwani vyeo hivyo havitakuwa na maana ikiwa wananchi hawapati huduma wanayoitarajia kutoka katika serikali waliyoiweka madarakani.

“Sisi viongozi wa Serikali lazima tufanye kazi kwa kujituma na kujitoa na tukumbuke kuwa sisi ni watumishi tu, sio watu wa kujivuna ama wabinafsi na kujinadi kwa vyeo vyetu kwamba mimi meneja, daktari sijui nani, vyeo vyetu vitakuwa na maana pale tu tunapokwenda kwa wananchi na kuwapa huduma” Alieleza.

Na kuongeza kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kuhakikisha kuwa kila kiongozi anayehudumia wananchi anakuwa mtumishi wa wananchi na kuhakikisha kuwa haki inatendeka na kuonya vikali watumishi wanaowahudumia wananchi kwa kutumia lugha chafu.   

Ameyasema hayo kwenye kikao cha muda mfupi kilichowajumuisha viongozi kutoka katika mashirika ya umma, wakala na mamlaka mbalimbali za serikali zilizomo Mkoani humo ili kufahamu matatizo wanayokumbana nayo pindi wanapotimiza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi.

Sambamba na hayo Mh. Wangabo amewataka watumishi wote Mkoani humo kuzingatia muda na kutekeleza kwa wakati mipango waliyojiwekea ili kazi zizae matunda na kutoa taarifa sehemu husika bila ya kusubiri kusukumwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo akifafanua namna mtumishi anavyotakiwa kuwajibika pindi anapowahudumia wananchi  (aliyekaa) kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa David Kilonzo. 
 Viongozi wa mashirika ya ya umma na mamlaka mbalimbali za seikali Mkoani Rukwa Waliohudhuria kwenye kikao hicho kilichowakutanisha wakuu wa mamlaka na mashirika ya umma. 



Hivyo makala RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi

yaani makala yote RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/rc-rukwa-awaasa-watumishi-kutotumia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi"

Post a Comment