title : RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA TAMASHA LA FIESTA KWA MASHARTI.
kiungo : RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA TAMASHA LA FIESTA KWA MASHARTI.
RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA TAMASHA LA FIESTA KWA MASHARTI.
Mh Makonda akizungumza na mgonjwa aliyepata huduma ya upimaji na Upasuaji wa jicho katika Meli ya Madktari kutoka China.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.PAUL MAKONDA amesema Serikali inaweka utaratibu wa kuendelea kuwahudumia Wagonjwa waliotibiwa ndani ya Meli ya Jeshi la China pindi Meli hiyo itakapoondoka wakiwemo wale waliofanyiwa Upasuaji na kuonekana wanahitajika kuendelea kupewa Matibabu hadi hapo watakapopona.
MAKONDA amesema kundi la Pili litakalohudumiwa ni Wale waliopatiwa matibabu lakini kuna Dawa watatakiwa kuendelea kuzipata Serikali itaweka utaratibu wa kuendelea kutoa Dawa hizo Bure hadi wapone.
Aidha MAKONDA amesema watu wote waliopatiwa Namba za Matibabu watahudumiwa pasipo usumbufu wowote.
Amesema idadi kubwa ya watu waliojitokeza kupima Afya haimaanishi kwamba Watanzania ni wagonjwa Bali ni mwitikio wa watu kutoka mikoani na nje ya Nchi waliofuata huduma hiyo.
Lengo la Serikali kutoa huduma ya Matibabu Bure ni kuwawezesha wasiokuwa na kipato kuweza kupata matibabu ili kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kutomudu gharama za matibabu.
Ameishukuru Serikali ya China kwa upendo walioonyesha kwa Wagonjwa waliokwenda kutibiwa Bure Hali inayodhihirisha Ukomavu wa Mahusiano baina ya Tanzania na China.
Katika Mazungumzo hayo Makonda aliwataka Clouds kuchagua Kati ya kufanya Tamasha hilo kwenye Uwanja wa Uhuru ili wapige Mziki hadi Asubuhi au kufanya kwenye Viwanja vya Leaders Club Clouds ambapo Clouds walichagua kufanya Tamasha hilo Viwanja vya Leaders Club na wapo tayari kufuata Sharti la kutoongeza Muda waliokubaliana.
" Baada ya Tamasha sitoruhusu tena Viwanja vya Leaders Club kutumika kwa Matamasha ya Usiku kwakuwa ni Usumbufu wa Wakazi na Ofisi za Bilozi zilizopo jirani na Viwanja hivyo"
Amesema kuwa Viwanja hivyo kwa sasa vitatumika kwa Matukio ya Nyakati za Mchana pekee hivyo kwa anaetaka kufanya Tamasha la kukesha atumie Uwanja wa Uhuru ambao umefunikwa na haupo karibu na Makazi ya Watu.
Amewataka Wananchi kufuata Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali na kusisitiza kuwa Sheria haina upendeleo kwa yoyote.
Amewasihi Wadau wa maendeleo kuwekeza katika Ujenzi wa Kumbi kubwa zenye Soundproof na uwezo wa kubeba watu Wengi ili zitumike kwenye matamasha ya kukesha.
Hivyo makala RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA TAMASHA LA FIESTA KWA MASHARTI.
yaani makala yote RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA TAMASHA LA FIESTA KWA MASHARTI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA TAMASHA LA FIESTA KWA MASHARTI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/rc-makonda-aongeza-muda-wa-tamasha-la.html
0 Response to "RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA TAMASHA LA FIESTA KWA MASHARTI."
Post a Comment