title : Rais Magufuli Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Leo
kiungo : Rais Magufuli Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Leo
Rais Magufuli Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Leo
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inakutana jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti Rais John Magufuli.
Kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika leo Jumatatu Novemba 20,2017 kitafuatiwa na kingine cha Halmashauri Kuu ya Taifa kesho Jumanne Novemba 21,2017.
Taarifa iliyotolewa awali na Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM, Humphrey Polepole imesema vikao hivyo pamoja na mambo mengine vitakuwa na ajenda ya kupokea tathmini ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 ambao kampeni zake zinaendelea.
“Ajenda nyingine ya vikao hivi vya uongozi vya kitaifa itakuwa kupokea, kuchuja, kutoa mapendekezo na kufanya uteuzi wa mwisho katika ngazi ya mikoa na taifa katika chama na jumuiya zake kwa maana ya umoja wa vijana, wanawake na wazazi,” ilisema taarifa ya Polepole.
CCM sasa ipo katika mchakato wa uchaguzi wa ndani kuanzia ngazi ya shina mpaka taifa
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akithibitisha kutimia kwa akidi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam kinachoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Novemba 20, 2017
Hivyo makala Rais Magufuli Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Leo
yaani makala yote Rais Magufuli Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Leo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais Magufuli Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Leo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/rais-magufuli-kuongoza-kikao-cha-kamati.html
0 Response to "Rais Magufuli Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Leo"
Post a Comment