RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA

RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA
kiungo : RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA

soma pia


RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA

pic%252Bpower%252Bbills
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 15 Novemba 2017, amerejea jijini Dar es salaam akitokea kijijini kwake Chato, mkoani Geita.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dare es salaam, Mhe. Rais amepokelewa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine wa mkoa.

Baada ya kutoka Uwanja wa Ndege, Rais Magufuli akiwa ameongozana na Makamu wa Rais pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, amekagua Ujenzi wa Daraja la juu Tazara ( Tazara Fly-Over) na Ujenzi wa Daraja la ghorofa tatu la Ubungo ( Ubungo Interchange)

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Ubungo, Rais Magufuli amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Ndyamukama Julius kuvunja sehemu ya jengo la TANESCO na jengo la Wizara ya Maji yaliyopo katika eneo la hifadhi ya barabara ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya daraja hilo.

”Sheria ya hifadhi ya barabara katika eneo hilo ni mita tisini kila upande kutoka katikati ya barabara hivyo ni lazima sheria hiyo iheshimiwe ili kuharakisha ujenzi wa Daraja la ghorofa tatu katika eneo hilo la Ubungo uanafanyika bila vikwazo kwani sheria ni msumeno haina budi kuzingatiwa hata na Serikali yenyewe” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameiagiza TANROADS kutangaza tenda ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita kumi na sita (16) kutoka eneo linapoishia Daraja la ghorofa tatu katika eneo la Ubungo kuelekea Chalinze ili itanuliwe kwa lengo la kurahisha usafiri katika jiji la Dar es salaam.

Rais Magufuli amewataka Makandarasi wanaojenga Daraja la Tazara na Ubungo kuharakisha ujenzi wa madaraja hayo usiku na mchana ili yaweze kumalizika kwa wakati ama kabla ya muda huo katika kurahisisha maendeleo ya kibiashara katika jiji la Dar es salaam.

”Dar es salaam ni jiji la kibiashara hivyo hakuna budi miundombinu yake ya usafiri iweze kurahisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka ndani ya jiji na nje ya jiji la Dar es salaam” amesema Rais Magufuli.

Mhandisi wa Masuala ya Usalama wa Ujenzi Mhandisi Richard Baruani amemueleza Rais Magufuli kuwa Ujenzi wa Daraja la Tazara umefikia asilimia 64 ambapo Daraja hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2018.

Kwa upande wa Daraja la ghorofa tatu la Ubungo, Mhandisi Mshauri Reginald Kayanga amesema ujenzi wake unatarajiwa kuanza rasmi Desemba 2017.

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam


15 Novemba, 2017


Hivyo makala RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA

yaani makala yote RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/rais-magufuli-aagiza-jengo-la-makao.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RAIS MAGUFULI AAGIZA JENGO LA MAKAO MAKUU YA TANESCO DAR KUVUNJWA"

Post a Comment