NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI

NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI
kiungo : NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI

soma pia


NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na maofisa wa forodha wa Sirari wilayani Tarime, kuongeza juhudi katika kulinda rasirimali ili kuunga mkono kasi ya Rais Dk John Mafuguli ya kulinda rasirimali hizo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka maofisa wa forodha wa Sirari wilayani Tarime kuongeza juhudi katika kulinda rasirimali ili kuunga mkono kasi ya Rais Dk John Mafuguli ya kulinda rasirimali hizo.

Ulega ameeleza hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa forodha hiyo katika kikao kati yake na watendaji baada ya kufanya ziara katika eneo hilo.
Alitoa kauli hiyo, baada ya kuelezwa kwamba wilaya hiyo haina tatizo la mifugo kutoka nje ya nchi na kuingia nchini lakini kumekuwa na tabia kwa baadhi ya madalali kutorosha mifugo na kuuza nchi jirani ya Kenya.

“Hili halikubaliki kabisa… kwa sababu kama Serikali tunakosa mapato yanayotokana na mifugo hii, na endapo ingekuwa inafuata utaratibu wa kupita katika forodha ya hii, tungepata mapato lakini  badala yake inapitishwa kwa njia za panya hadi Kenya”. Alisema Ulega.

Aliwaataka watendaji hao kutobabaika badala yake wasimamie sheria na kufanya kazi kwa uadilifu ikiwamo kushirikiana ili kudhibiti hali hiyo ambayo inarudisha nyuma jitihada za Serikali za kuleta maendeleo.

Pia Ulega alitumia nafasi hiyo kuwaeleza watumishi hao kwamba wizara itahakikisha kituo cha ukaguzi wa mifugo cha Kirumi wilayani Butiama kinafanya kazi kwa ufanisi kwa kuweka miundombinu ya maji na umeme ili mnada uliopo uanze kufanya kazi.

Kabla ya kwenda katika forodha hiyo, Ulega alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na walipeana mikakati mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha sekta ya mifugo na uvuvi inasonga mbele.

Katika mazungumzo yao viongozi hao walikubaliana suala la kudhibiti uvuvi haramu hasa unaofanyika katika ziwa Victoria ambapo Malima alimuahidi Ulega kwamba atahakikisha anatumia vyombo vya dola ili kukabiliana na hali hiyo.

Wakati Malima akieleza hayo, Ulega naye alimuhakikishia kwamba wizara hiyo itakuwa bega kwa bega kushirikiana na mkoa huo katika kuhakikisha sekta hizo zinapiga hatua na kusonga mbele.

Mbali na hilo, viongozi hao walikubaliana kuanza kwa mchakato wa kufufua viwanda vya kusindika samaki na nyama vilivyopo ili kuunga mkono jitihada za Dk Magufuli za Tanzania ya viwanda
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima alipo wasili juu ya mikakati mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha sekta ya mifugo na uvuvi inasonga mbele.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na watendaji wa wilaya ya Rorya wakati alipofanya ziara kutembelea na kupata taarifa ya hali ya mifugo na uvuvi katika wilaya hiyo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Mara.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa forodha ya Sirari wilayani Tarime.



Hivyo makala NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI

yaani makala yote NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/naibu-waziri-ulega-awataka-maofisa-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA MAOFISA WA FORODHA TARIME KUONGEZA JUHUDI ZA KULINDA RASIRIMALI"

Post a Comment