title : MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI
kiungo : MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI
MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI
Na Mathias Canal, Mbeya
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana Novemba 29, 2017
amemuagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kumsimamisha
kazi Afisa Kilimo Wilaya ya Mbeya anayesimamia zao la Pareto Ndg
Emmanuel Halinga ili kupisha uchunguzi.
Mhe
Naibu Waziri ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi
Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania mara baada ya Mhe
Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Oran Njeza na Wananchi wote waliokuwepo kwenye
mkutano huo wa hadhara kumrushia shutuma nzito na kumkataa mtaalamu huyo
wa kilimo mbele ya Naibu Waziri.
Alisema
kuwa pamoja na zao hilo la Pareto kuwa la kwanza kwa uzalishaji katika
nchi za Afrika huku likiwa zao la pili kwa uzalishaji Duniani lakini
bado halijamkomboa Mkulima nchini jambo ambalo linaonyesha namna ambavyo
baadhi ya wataalamu Wa Kilimo wameshindwa kutekeleza majukumu yao
ipasavyo.
Alisema
kuwa wataalamu wa kilimo walipaswa kusimamia kwa kiasi kikubwa zao hilo
kwani Pato lake ni wastani wa tani 2000 kwa mwaka sawa na Bilioni 12
mpaka 14 ambapo katika kipindi hili bei ya kuanzia Mkulima analipwa
shilingi 2300 kwa kilo lakini inapanda mpaka shilingi 3300 kulingana na
ubora wa zao hilo ambalo mkulima amelima.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017. Picha zote Na Mathias Canal
Hivyo makala MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI
yaani makala yote MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/mwanjelwa-amuagiza-mkurugenzi_30.html
0 Response to "MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI"
Post a Comment