MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI

MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI
kiungo : MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI

soma pia


MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana Novemba 29, 2017 amemuagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kumsimamisha kazi Afisa Kilimo Wilaya ya Mbeya anayesimamia zao la Pareto Ndg Emmanuel Halinga ili kupisha uchunguzi.

Mhe Naibu Waziri ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania mara baada ya Mhe Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Oran Njeza na Wananchi wote waliokuwepo kwenye mkutano huo wa hadhara kumrushia shutuma nzito na kumkataa mtaalamu huyo wa kilimo mbele ya Naibu Waziri.

Alisema kuwa pamoja na zao hilo la Pareto kuwa la kwanza kwa uzalishaji katika nchi za Afrika huku likiwa zao la pili kwa uzalishaji Duniani lakini bado halijamkomboa Mkulima nchini jambo ambalo linaonyesha namna ambavyo baadhi ya wataalamu Wa Kilimo wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Alisema kuwa wataalamu wa kilimo walipaswa kusimamia kwa kiasi kikubwa zao hilo kwani Pato lake ni wastani wa tani 2000 kwa mwaka sawa na Bilioni 12 mpaka 14 ambapo katika kipindi hili bei ya kuanzia Mkulima analipwa shilingi 2300 kwa kilo lakini inapanda mpaka shilingi 3300 kulingana na ubora wa zao hilo ambalo mkulima amelima.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017. Picha zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mhe Oran Njeza akizungumza katika mkutano huo kufikisha kilio cha wananchi mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwwa kuhusu zao la Pareto na matatizo la wafanyabiashara kujaza Lumbesa kwenye uuzaji wa mazao mbalimbali likiwemo zao la viazi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini Jojo Kata ya Santilya, Jana Novemba 29, 2017.





Hivyo makala MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI

yaani makala yote MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/mwanjelwa-amuagiza-mkurugenzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI"

Post a Comment