MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21

MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21
kiungo : MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21

soma pia


MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21


Na Mathias Canal, Mbeya

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo amewasihi wananchi kwa kauli moja kuchagua kiongozi makini anayetokana na CCM.

Mhe Mwanjelwa alisema kuwa kumchagua diwani wa CCM ni dalili nzuri ya kumpongeza na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anazozifanya kwa muktadha wa kuwaletea maendeleo watanzania wote.

Mjumbe huyo wa NEC, aliyasema hayo Leo Novemba 20, 2017 katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Bujinga A na B kilichopo Kata ya Ibigi, Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya ambapo alimnadi mgombea Udiwani wa Kata hiyo Bi Suma Ikenda Fyandomo.

(Mnec), Mhe Mwanjelwa aliwakumbusha wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kuwa Hawachagui ilani mpya Bali wanachagua Diwani kwa ajili ya kutekeleza ilani ya Ushindi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 ambayo wananchi waliiamini na kuichagua Octoba 25, 2015.

Alisema kuwa nchini Tanzania hakuna chama chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi Bali Chama Cha Mapinduzi pekee ndicho chenye uwezo na jukumu la kuwaletea maendeleo endelevu wananchi.

Katika Mkutano huo wanachama 21 walivutiwa na hotuba ya Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM wakati akimnadi mgombea hivyo kufanya maamuzi ya kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM ambapo wameahidi kushirikiana na mgombea udiwani wa CCM ili kuhakikisha anashinda kwa kishindo.

Ushiriki wa kampeni hizo katika Kata ya Ibigi unajili wakati ambapo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa yupo ziarani Mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine Kesho Disemba 21, 2017 atashiriki ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu Tawala na washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini juu ya mfumo wa ununuzi wa mbolea (BPS).

Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa Jijini Mbeya.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akimvalisha kofia ya CCM kijana aliyehama Chadema wakati wa kampeni za Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akifurahi na wananchama wa CCM wakati wa mkutano wa kumnadi Mgombea Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akifurahi na wananchama wa CCM wakati wa mkutano wa kumnadi Mgombea Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017.


Hivyo makala MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21

yaani makala yote MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/mwanjelwa-amnadi-mgombea-udiwani-kata.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21"

Post a Comment