title : MBEGU YA MAHINDI YA WEMA 2109 NA MIHOGO ILIYOTOLEWA NA COSTECH WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA KUONGEZA CHACHU YA KILIMO
kiungo : MBEGU YA MAHINDI YA WEMA 2109 NA MIHOGO ILIYOTOLEWA NA COSTECH WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA KUONGEZA CHACHU YA KILIMO
MBEGU YA MAHINDI YA WEMA 2109 NA MIHOGO ILIYOTOLEWA NA COSTECH WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA KUONGEZA CHACHU YA KILIMO
Na Dotto Mwaibale, Mbogwe, Geita.
MAKAMU Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Nsika Sizya amesema mbegu bora ya mahindi ya WEMA 2109 na mihogo aina ya Mkombozi waliyokabidhiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) itaongeza chachu ya kilimo wilayani humo.
Sizya aliyasema hayo wilayani humo jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema yanayostahimili ukame na mihogo kwa ajili ya mashamba darasa kwa wakulima wa vijiji vinne vya Mponda kilichopo Kata ya Luganga, Kijiji cha Ushetu kilichopo Kata ya Ushirika, Kijiji cha Lwazeze kilichopo Kata ya Ngemo na Kijiji cha Iponya kilichopo Kata ya Iponya.
Alisema changamoto kubwa waliyokuwa nayo wakulima katika Halmshauri hiyo ni kukosekana kwa mbegu bora za mihogo na mahindi ambapo alisema kwa kupata mbegu hizo kutaongeza ari na chachu ya kilimo kwa wananchi.
Aliishukuru CSTECH na OFAB kwa kuwapelekea mradi huo katika wilaya hiyo na kuupokea kwa shangwe kwa kuzingatia kuwa mihogo ni zao la biashara na chakula ambapo aliwataka wananchi kubadilika na kufanya kilimo chenye tija kama wataalamu wanavyowaelekeza.
Mkulima wa Kijiji cha Lwazeze, Charles Kangai akichimba mashimo kwa ajili ya upandaji mbegu ya mahindi ya WEMA.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula, akielekeza jinsi ya upandaji wa mbegu hiyo ya mihogo aina ya Mkombozi. Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Nsika Sizya, akipanda mbegu ya mihogo katika shamba darasa katika Kijiji cha Iponya.
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange, akipanda mbegu ya mihogo aina ya Mkombozi kwenye shamba darasa katika Kijiji cha Iponya.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MBEGU YA MAHINDI YA WEMA 2109 NA MIHOGO ILIYOTOLEWA NA COSTECH WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA KUONGEZA CHACHU YA KILIMO
yaani makala yote MBEGU YA MAHINDI YA WEMA 2109 NA MIHOGO ILIYOTOLEWA NA COSTECH WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA KUONGEZA CHACHU YA KILIMO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBEGU YA MAHINDI YA WEMA 2109 NA MIHOGO ILIYOTOLEWA NA COSTECH WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA KUONGEZA CHACHU YA KILIMO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/mbegu-ya-mahindi-ya-wema-2109-na-mihogo.html
0 Response to "MBEGU YA MAHINDI YA WEMA 2109 NA MIHOGO ILIYOTOLEWA NA COSTECH WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA KUONGEZA CHACHU YA KILIMO"
Post a Comment