title : MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA YADHIBITIWE
kiungo : MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA YADHIBITIWE
MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA YADHIBITIWE
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima kwenye Halmashauri ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa kongamano la siku mbili la Chama cha Wahasibu Tanzania(TAA) lililojumuisha wataalam wa Hesabu na wafanya maamuzi kutoka katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Katika Kongamano hilo ambalo Linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Chama hicho mwaka 1983 limelenga kujenga uwezo kuhusu Uwazi na Uwajibikaji kwa Viongozi waandamizi wa Mamlaka ta Serikali za Mitaa katika Matumizi ya Fedha za Umma.
Waziri Jafo amesema kuwa Bajeti kubwa ya Serikali inapelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa takribani asilimia 20.7 ya Bajeti ya Serikali huelekezwa katoka Halmashauri hivyo ni eneo ambalo linapata Fedha nyingi na zinahitajo uangalizi mkubwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selamani Jafo akifungua kongamano ya Chama cha Wahasibu Tanzania linalohusu uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa linalofanyika Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania Fred Msemwa akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa Kongamano linalohusu uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Washiriki na wajumbe wa chama cha Wahasibu Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Ufunguzi wa Kongamano lililofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Mhe.Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo(kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania Fred Msemwa wakati wa Ufunguzi wa Kongamano linalofanyika Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo(Katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wahasaibu Tanzania pamoja na wawwezeshaji wa Kongamano hilo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA YADHIBITIWE
yaani makala yote MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA YADHIBITIWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA YADHIBITIWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/matumizi-yasiyo-ya-lazima-yadhibitiwe.html
0 Response to "MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA YADHIBITIWE"
Post a Comment