Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara

Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara
kiungo : Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara

soma pia


Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara






Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara akisisitiza jambo kwa wenye wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mtwara na baadhi ya wageni waalikwa kwenye sherehe za uzinduzi wa zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara ambalo linatarajiwa kuanza rasmi mwanzoni mwa wiki ijayo

Kaimu mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa NIDA Bi. Rose Joseph akiwasilisha salamu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndg, Andrew Wilson Massawe kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo wakati wa zoezi la uzinduzi wa usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mtwara na kuhudhuriwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, watumishi wa NIDA pamoja na wageni wengine waalikwa.

Baadhi ya Wakuu wa Wilaya na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa pichani wakisikiliza jambo kutoka kwa mwakilishi Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakati wa sherehe ya uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Mtwara pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara wakati wa zoezi la uzinduzi wa usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara

Afisa usajili msaidizi wa NIDA Ndg. Fredy Mahundi akifanya zoezi la usajili kwa mara ya kwanza kwa mwananchi wa mkoa wa Mtwara mara baada ya zoezi la uzinduzi wa usajili kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara kukamilika.

Bi Amina Bakari akichukuliwa alama zake za Vidole ambapo alipata nafasi ya kuwa mwananchi wa kwanza kusajiliwa kwa mkoa wa Mtwara mara baada ya zoezi la uzinduzi wa usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa mkoa wa Mtwara kukamilika.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo amezindua rasmi zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa wananchi wa mkoa huo tayari kuanza rasmi kwa zoezi la usajili kwa wananchi ikihusisha kuchukuliwa picha, saini na alama za Kibaiolojia.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Mtwara umejipanga na uko tayari kwa zoezi hilo, na kuahidi kutoa ushirikiano kwa hali na mali kuhakikisha hakuna mwananchi yeyote mwenye sifa ambaye ataachwa bila kusajiliwa.


Katika sherehe za uzinduzi rasmi wa zoezi hilo zilizofanyika makao makuu ya Mkoa huo Mtwara; zilihudhuriwa na Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Meya, Katibu Tawala Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri zote, Makatibu Tawala wa Wilaya, Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ngazi ya Mkoa, Watumishi katika ngazi mbalimbali na vyombo vya Habari.


Akizungumza kwa niaba ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Rose Joseph ameeleza Mamlaka imejipanga kuanza rasmi zoezi hilo Jumatatu tarehe 13 Novemba, 2017 na wanakusudia kukamilisha zoezi hilo kwa mkoa wa Mtwara kufikia Februari 2018 na kuanza kutoa namba za Utambulisho NIN sambamba na uzalishaji wa Vitambulisho.


Ziadi ya wananchi mil 1,250,000 wanatazamiwa kusajiliwa mkoani humo. Mikoa mingine ambayo usajili umeanza ni Njombe, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Arusha, Shinyanga, Geita, Mwanza, Simiyu, Manyara na Songwe.


Hivyo makala Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara

yaani makala yote Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/matukio-uzinduzi-wa-zoezi-la-usajili-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Matukio : Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wafanyika , Manyara"

Post a Comment