MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA

MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA
kiungo : MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA

soma pia


MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS Nchini akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili kulia) alipowasili kwenye katika Ukumbi wa  Chuo cha Mipango Dodoma tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo 30 Novemba, 2017 hapa mjini Dodoma. 

Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS) kimefanya Mkutano wake Mkuu wa Tano wa Mwaka 2017 kwa ufanisi Mkoani Dodoma.
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,  Miyuji Dodoma leo Novemba 30,  2017.

Akiongea katika Mkutano huo Kaimu Naibu  Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw.  Charles Malunde kwa niaba ya Naibu Mrajisi ametoa angalizo kwa Vyama vya ushirika nchini kutokufanya biashara za Kibenki nje ya lengo la kuanzishwa kwa SACCOS.

Amesema kuwa katika  vyama vingi vya ushirika uzoefu umeonesha kuwa wakishakuwa na mtaji mkubwa huwa na wazo la kuanzisha Benki, ametoa angalizo kuwa masharti ya uendeshaji wa Benki ni tofauti kabisa na masharti ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hivyo ameziasa Saccos zote nchini kutafakari vyema kabla ya kubadili vyama hivyo na kuwa Benki.
“ Ukianzisha Benki huduma za Saccos zitafifia, kumbukeni wateja wa Saccos ni pamoja na wale wa hali ya chini kabisa ikiwa benki hawa huenda mkawaacha” alisisitiza  Kaimu Mrajis Malunde.

Aidha,  amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria  lakini pia kuheshimu na kusikiliza sana wenye mali ambao ni wanachama wa vyama hivyo vya ushirika.
Aliongeza kuwa kwakuwa Mkutano huu utahusisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi Bw. Charles Malunde pia amewaasa Wajumbe wa Mkutano Mkuu kuwa makini katika uchaguzi huo kwa kuchagua watu wenye weledi na wenye mapenzi ya dhati na ushiriki wao ili waweze kutimiza majukumu yanayokusudiwa.

Pia amewataka wagombea wote wanaowania nafasi mbalimbali za chama hicho kujiuliza mambo manne kama ifuatavyo;- Je, watumishi wa Jeshi la Magereza wote ni wanachama? na mnaweka Mkakati gani?, Je wanachama wanaweka akiba za kila mwezi?, Mnajiendesha kisayansi? Mtu akitaka mkopo anapata baada ya muda gani? na swali la mwisho uhusiano na vyama vingine vya ushiriki, SCULT, nje ya nchi ukoje?.

Awali akitoa taarifa ya Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS), Mwenyeki wa Bodi ya Magereza Saccos, DCP. Gideon Nkana amesema kuwa Idadi ya wanachama imeongezeka hadi kufikia wanachama zaidi ya 13,000 ikiwa na mtaji wa zaidi ya bilioni 18.
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(katikati) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS kuingia Ukumbini tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Hivyo makala MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA

yaani makala yote MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/magereza-saccos-yafanya-mkutano-mkuu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA"

Post a Comment