title : MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI
kiungo : MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI
MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni .kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Mnadani ,Nasib Mdeme,Diwani wa kata ya Weruweru ,Swaleh Msenges na Diwani wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi ,Wengine katika picha ni kulia mwa msimamizi wa uchaguzi ni Msimaizi Msaidizi na Mkuu wa Idara ya Fedha Juma Massatu na kushoto ni Afisa Uchaguzi wilaya ya Hai,Edward Ntakiliho.
Madiwani waliochaguliwa hivi karibuni wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Hai wakiwa na ndugu zao.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .
MSIMAMIZI wa uchaguzi katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro ,
Ndugu Yohana Sintoo amesema kuwa zoezi la uchaguzi katika kata tatu zilizokuwa
hazina uwakilishi limekamilika salama na kuwapata viongozi watakaowawakilisha
wananchi kwenye kata husika.
Ndg Sintoo ameyasema hayo wakati akikabidhi vyeti kwa madiwani
wateule watatu walioshinda kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba
26 mwaka huu.
“Ndugu zangu mtakumbuka kuwa mwishoni mwa wiki kulikuwa na
uchaguzi kwenye jimbo letu ambapo wananchi wa kata tatu walikuwa katika zoezi
la upigaji kura kwa lengo la kuwapata viongozi wa ngazi ya udiwani baada ya
madiwani wa kata husika kujiuzulu”
“Wananchi wa kata za Mnadani , Weruweru na Machame Magharibi
walipiga kura ili kuwapata wawakilishi wao ambapo zoezi hilo limekamilika
bila uvunjifu wa amani kuanzia kipindi cha mikutano ya kampeni hadi
siku ya zoezi la upigaji kura na leo tunawapatia washindi vyeti vyao”
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Weruweru Swalehe Msenges.kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri hiyo ,Juma Massatu.
Hivyo makala MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI
yaani makala yote MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/madiwani-wa-ccm-walioshinda-katika_29.html
0 Response to "MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI"
Post a Comment