title : Mabosi wa Kampuni wa inayojenga Uwanja wa Mao watinga Zanzibar, Sasa uwanja huo utakamilika June 2018
kiungo : Mabosi wa Kampuni wa inayojenga Uwanja wa Mao watinga Zanzibar, Sasa uwanja huo utakamilika June 2018
Mabosi wa Kampuni wa inayojenga Uwanja wa Mao watinga Zanzibar, Sasa uwanja huo utakamilika June 2018
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo imepokea viongozi wakuu wa kampuni ya Zhengtar Group Company Limited ya nchini China ambayo ndio inayojenga viwanja vya Michezo vya Mao Tse Tung.
Viongozi hao wamekutana na Waziri wa Wizara hiyo Rashid Ali Juma kufanya mazungumzo na baadae kuangalia kazi za ujenzi wa viwanja hivyo unavyoendelea huko Mao Tse Tung .
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Omar Hassan “King” amesema kwa mujibu wa viongozi hao kazi ya ujenzi wa uwanja huo inatarajiwa kukamilika kama makubaliano ya mkataba yalivoelekeza.
Amesema kwa mujibu mkataba baina ya kampuni hiyo na wizara uwanja huo ulikuwa ukamilike mwezi wa tatu mwakani kwa kazi za awali lakini kutokana na kuchelewa kwa vifaa vya ujenzi huo unaweza kuchelewa kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu ya ziada.
Hata hivyo Kingi amesema kutokana na hali ya haraka unavyokwenda ujenzi wa uwanja huo unatazamiwa utakamilika mwezi wa June hadi July mwaka 2018.
Uwanja huo utakuwa na Viwanja viwili vya mpira wa miguu na chengine cha michezo ya ndani kama vile Mpira wa Kikapu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Pete na mengineyo.
Katika Viwanja hivyo vya Mpira wa Miguu uwanja mmoja utakuwepo upande wa Magharibi ambao utakuwa na Jukwaa moja litakalochukuwa Mashabiki 1500 waliokaa huku uwanja mwengine wa mpira wa miguu utakuwepo upande wa Mashariki ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua Mashabiki waliokaa 900 katika jukwaa moja ambalo litakuwepo katika Uwanja huo, pia Viwanja hivyo vitakuwa na taa ambazo zitaweza kuwezesha kuchezwa michezo hadi usiku.
Hivyo makala Mabosi wa Kampuni wa inayojenga Uwanja wa Mao watinga Zanzibar, Sasa uwanja huo utakamilika June 2018
yaani makala yote Mabosi wa Kampuni wa inayojenga Uwanja wa Mao watinga Zanzibar, Sasa uwanja huo utakamilika June 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mabosi wa Kampuni wa inayojenga Uwanja wa Mao watinga Zanzibar, Sasa uwanja huo utakamilika June 2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/mabosi-wa-kampuni-wa-inayojenga-uwanja.html
0 Response to "Mabosi wa Kampuni wa inayojenga Uwanja wa Mao watinga Zanzibar, Sasa uwanja huo utakamilika June 2018"
Post a Comment