title : KIJANA ANAYEDAIWA KUUA MTU ASIYEJULIKANA AFIKISHWA MAHAKAMANI
kiungo : KIJANA ANAYEDAIWA KUUA MTU ASIYEJULIKANA AFIKISHWA MAHAKAMANI
KIJANA ANAYEDAIWA KUUA MTU ASIYEJULIKANA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Na Karama Kenyunko wa Blogu ya Jamii
Kijana wa miaka 22, anayeishi Ipililo Maswa mkoani Shinyanga leo Novemba 24, 2017 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kumuua mtu asiyejulikana.
Kwa mujibu wa chanzo cha Habari cha uhakika kijàna huyo ambaye alikamatiwa katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam na alikutwa akiwa na viungo vya binadamu ambavyo ni sehemu za mbalimbali za siri za mwanamke na nyara za serikali.
Mshtakiwa Nkonja amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.
Wakili wa serikali Nassoro Katuga akisoma hati ya mashtaka amedai kati ya Oktoba Mosi na 30 mwaka huu katika eneo la Kahama Shinyanga na Kituo cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam, alimuua mtu ambaye bado hajafahamika.
Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Decemba 8, mwaka huu. Upelelezi bado haujakamilika
Hivyo makala KIJANA ANAYEDAIWA KUUA MTU ASIYEJULIKANA AFIKISHWA MAHAKAMANI
yaani makala yote KIJANA ANAYEDAIWA KUUA MTU ASIYEJULIKANA AFIKISHWA MAHAKAMANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIJANA ANAYEDAIWA KUUA MTU ASIYEJULIKANA AFIKISHWA MAHAKAMANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/kijana-anayedaiwa-kuua-mtu.html
0 Response to "KIJANA ANAYEDAIWA KUUA MTU ASIYEJULIKANA AFIKISHWA MAHAKAMANI"
Post a Comment